Mbowe, Lissu, Mnyika kuelekea Italia kwa ziara ya kikazi

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema imeeleza kuwa katika safari hiyo, Mbowe ameambatana na viongozi wengine wawili wa...

0

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania chama cha Chadema, Freeman Mbowe ameondoka nchini humo kuelekea Italia kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema imeeleza kuwa katika safari hiyo, Mbowe ameambatana na viongozi wengine wawili wa chama hicho, ambao ni Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu na Katibu Mkuu, John Mnyika.

Kwa mujibu wa Mrema kupitia taarifa hiyo Lissu na Mnyika watatangulia kurejea nchini Juni 7, mwaka huu wakati Mbowe akiendelea na ziara kwingineko.

Imeelezwa kuwa Mwenyekiti huyo baada ya kuhitimisha ziara ya Italia, atakwenda Ujerumani kwa ziara ya siku mbili.

Atakapokuwa Ujerumani kulingana na taarifa hiyo, atakutana na viongozi mbalimbali wa kisiasa, Serikali na Mashirika ya Kimataifa na kwamba atarejea nchini Juni 10 mwaka huu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted