Mwandishi nguri wa habari nchini Tanzania Leila Sheikh kuzikwa leo jijini Tanga

Leila ambaye atazikwa leo katika makaburi  ya Sharif Haidari na swala itafanyika katika msikiti mkuu wa Ijumaa jijini Tanga.aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji na miongoni mwa waanzilishi wa Chama...

0

Tasnia ya habari nchini Tanzania inaomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na mmoja wa waanzilishi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Leila Sheikh ambaye alifariki ghafla usiku wa kuamkia jana Jumatatu huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Leila ambaye atazikwa leo katika makaburi  ya Sharif Haidari na swala itafanyika katika msikiti mkuu wa Ijumaa jijini Tanga.aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji na miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania, TAMWA, kuanzia mwaka 1996 hadi 2001.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk. Rose Reuben amesema marehemu Leila atakumbukwa sana katika tasnia ya habari nchini na mchango wake mkubwa katika kutumia kalamu yale kuandika masuala mbalimbali ya haki za wanawake nchini.

“Leila Sheikh atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari na jinsia, tangu kuanzishwa kwa chama hiki,  Akiwa mmoja wa waasisi wakeamekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi mapana ya taifa katika mrengo wa jinsia na haki za wanawake na watoto kiujumla,”- amesema Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk. Rose Reuben

Leila Sheikh alikuwa mwanablogu, mwanaharakati na mtetezi wa haki za wanawake na watoto, na mhariri wa gazeti la Sauti ya Siti lililochapishwa na TAMWA.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted