Africa East Africa

Bei mpya za mafuta kuanza kutumika leo nchini Tanzania, huku bei ya mafuta ya Petrol ikishuka

Katika taarifa iliyotolewa jana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza kuwa bei kikomo zinazoanza leo Julai 5, 2023 kuwa bei za rejareja za mafuta ya petroli na dizeli yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeshuka kwa shilingi 137 kwa lita na shilingi 118 kwa lita, mtawalia ikilinganishwa na bei zilizotumika Juni.