Kibano wauza Sukari zaidi ya 3200

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Dkt Ashatu Kijaji amewataka Maafisa Biashara wote nchini humo kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei...

0

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Dkt Ashatu Kijaji amewataka Maafisa Biashara wote nchini humo kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.

Dkt Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo.

Amesema ni jukumu la Maafisa  Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua.

Dkt. Kijaji amesisitiza kuwa  ni jukumu  la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya Juhudi  za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na  mazingira bora na wezeshi  ili kukuza biashara zao na kiwa na tija. 

Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchinj zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.

Vilevile amekipongeza Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC kwa kutoa ajira zaidi ya elfu 3200 na jinsi kinavojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii inayokizunguka 

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted