Ocean Road waanza kutoa huduma ya urekebishaji wa mfumo wa nyongo iliyoziba pasipo upasuaji 

Huduma hiyo mpya imeanza kutolewa hivi karibuni na Wataalam wa Radiolojia tiba wakiongozwa na daktari bingwa na mbobezi wa radiolojia tiba Dkt. Latifa Rajab kutoka Taasisi ya Saratani...

0

Taasisi ya Saratani Ocean Road yaanza kutoa za Huduma za urekebishaji wa mfumo wa nyongo iliyoziba pasipo upasuaji ambapo mfumo huo unapoziba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo saratani kusababisha manjano na muwasho mkali mwili mzima pamoja homa kali wakati mwingine kwa mgonjwa husika. 

Huduma hiyo mpya imeanza kutolewa hivi karibuni na Wataalam wa Radiolojia tiba wakiongozwa na daktari bingwa na mbobezi wa radiolojia tiba Dkt. Latifa Rajab kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road baada ya daktari huyo kurejea kutoka masomoni. 

Aidha huduma hizi hufanywa kwa utaratibu wa mirija kupelekwa kwenye tumbo kwa kuangalia kupitia mashine ya x ray na ultrasound ili kuhakikisha mirija limefika na nyongo inaenda katika njia yake.
“Nyongo ikiwa nyingi inasabisha madaktari bingwa wa saratani kushindwa kumpa tiba mgonjwa huyu hivyo, kwa kupata huduma hii nyongo inashuka kuwa kawaida ndani ya siku chache kisha mgonjwa ataendelea na matibabu yake ya saratani na kumuepushia adha ya muwasho na manjano na pengine kifo kutokana na vimelea (bacteria) kuzaliana katika mirija ya nyongo iliyoziba”, ameeleza Dkt. Latifa. Dkt. Latifa amesisitiza kuwa sasa kazi imeanza na mambo yote yatamalizika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road hapa nchini.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted