Polisi nchini Tanzania wakabiliana na wakosoaji wa mkataba tata wa bandari huku idadi ya waliokamatwa ikiongezeka

Hadi sasa zaidi ya watu watatu wametajwa kukamatwa akiwemo Dk Willibrod Slaa, aliyewa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na mwanansiasa maarufu nchini humo na mmoja wa wakosoaji...

0

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linaendelea na msako wa wakosoaji wa Mkataba wa Bandari nchini humo hali iliyozua sintofahamu huku ukukwaji wa haki za binadamu ukitajwa kuwepo.

Hadi sasa zaidi ya watu watatu wametajwa kukamatwa akiwemo Dk Willibrod Slaa, aliyewa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na mwanansiasa maarufu nchini humo na mmoja wa wakosoaji kinara wa makubaliano ya uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na Dubai.

Anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi na uhaini, wakili wake amethibitisha. Dk Slaa amekamatwa siku ya jumapili jijini Dar es Salaam huku msako mkali dhidi ya wakosoaji wa mpango huo ukionekana kushika kasi nchini Tanzania. 

Hapo jana kwenye mitandao ya kijamii, kulisambaa taarifa kuwa Dk Slaa, alikamatwa nyumbani kwake, kabla ya kupelekwa Kituo cha Polisi Kawe kwa mahojiano.

Wakili wake, Bw. Dickson Matata amethibitisha kukamatwa kwa Dkt Slaa hapo jana na kuwa polisi walikuwa wakifanya upekuzi nyumbani kwake.

Mbali na Dk Slaa wengine waliokamatwa ni mwanasheria na mwanasiasa wa upinzani Boniface Anyasile Mwabukusi, Mpaluka Nyagali alimaarufu kama Mdude Nyagali ambaye ni mwanaharakati na kada wa Chadema pamoja na  Emmanuel Masonga, Katibu wa Kanda ya Kati wa Chadema.

Wote kwa pamoja wamekamatwa kwa tuhuma za uchochezi na kupanga maandamano ya nchi nzima yenye lengo la kuiangusha serikali.

Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya tamko la Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Camillus Wambura, alilolitoa Agosti 11,2023 kuhusu kuchukua hatua dhidi ya kundi linalopanga kufanya maandamano nchini kote ili kuiangusha serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025.

“Hili halivumiliki,” Wambura aliwaambia waandishi wa habari. “Haitawahi kuwa. [Watu hawa] wamefikia hatua ya hatari sana. Tutawapata na kuwafikisha mbele ya sheria. Uasi na uhaini ni uhalifu unaoweza kuadhibiwa katika nchi yetu, na hatutaacha hili liendelee bila kuingiliwa.”IGP Camillus Wambura

Ukandamizaji unaoendelea kufanywa na polisi unakuja huku kukiwa na ukosoaji kwamba mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikichukua hatua zinazotafsiriwa kuwanyamazisha wakosoaji wa mkataba tata wa bandari ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameutetea, akiuelezea kuwa ni “fursa adimu.Mapema wiki hii, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch liliripoti kwamba mamlaka “imewaweka kizuizini au kuwatishia” takriban watu 22 tangu Juni 10, 2023, kwa kushirikiana na upinzani wao dhidi ya makubaliano hayo, na kuitaka Tanzania “ikomeshe ukamataji huu wa kiholela na kuchukua hatua zaidi kushughulikia. changamoto za uhuru wa kujieleza.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted