Awanywesha sumu watoto wa mume wake kisa pesa ya mtumizi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Agosti 12, 2023 saa tatu usiku katika kijiji na kata ya Itobo Wilaya ya Nzega ambapo...

0

Watoto wawili wa familia moja, Dickson Zakaria (5) na Goodluck Zakaria (4) wamefariki baada ya mama yao wa kambo kuwanywesha dawa ya kuulia wadudu kwenye mazao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Agosti 12, 2023 saa tatu usiku katika kijiji na kata ya Itobo Wilaya ya Nzega ambapo watoto hao walikorogewa sumu na mama huyo (jina limehifadhiwa) kisha nayeye kunywa sumu hiyo.

Abwao ametaja chanzo cha tukio hilo ni baada ya baba wa watoto hao aitwaye Zakaria Dotto kudaiwa kutotoa fedha za matumizi na kusababisha mzozo uliopelekea kukimbia kuukwepa.

Kitendo hicho kinadaiwa kumuudhi mama huyo aliyeamua kukoroga sumu ya dawa ya kuulia wadudu kwenye mazao na kuwanywesha watoto hao na yeye kuinywa.

Baba wa watoto hao aliporudi nyumbani kwake alikuta hali ya mkewe si nzuri ndipo alipomkimbiza hospitali pasipokujua chochote kuhusu watoto wake.

“Alimkuta mkewe katika hali isiyonzuri baada ya kunywa sumu na kumpeleka hospitali kisha kurudi nyumbani kwake,”  amesema

Kamanda Abwao amesema baba huyo alienda kuwaangalia watoto wake na kuwakuta tayari wamefariki,  kisha kurudi hospitali na kumuuliza mke wake kuhusiana na watoto hao na kujibiwa kuwa amewapa sumu.

Abwao amesema mama huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwaajili ya uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.

Ametoa wito kwa wana ndoa na wenye mahusiano kupeleka changamoto zao kwa viongozi wa dini au Serikali na sio kujichukulia sheria mkononi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted