Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la unajisi na kumwingilia kinyume na maumbile binti wa miaka 9

Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha jela Ezekia Mwaitoto Msawile (45) mkazi wa Ilemi jijini Mbeya baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya...

0

Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha jela Ezekia Mwaitoto Msawile (45) mkazi wa Ilemi jijini Mbeya baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya unajisi na kumwingilia kinyume cha maumbile mtoto wa miaka tisa. 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo mkoani Mbeya Zawadi Laizer baada ya kumaliza kusikiliza ushahidi wa mashahidi kadhaa wa Jamhuri na upande wa utetezi na kuridhishwa na ushahidi wa jamuhuri ambao unaelezwa kutoacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili. 

Hakimu Laizer amesema Mahakama yake haijapata mashaka na mshtakiwa Ezekia Mwaitoto kutenda makosa hayo mawili kama ambavyo pia kwenye utetezi wake hakuwa na cha kujitetea kwenye kesi hiyo namba 06/2023. 

Mwendesha mashtaka wa Serikali George Ngwembe ameiomba Mahakama kutoa adhabu stahiki kama sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na watu wengine kwenye jamii na maombi ya mwanasheria wa Serikali yanatolewa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu wanaoamini imani za kishirikina kwa kwenda kutembea au kuwabaka watoto na vikongwe ili wapate utajiri. 

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Mshtakiwa Ezekia Mwaitoto Msawile anadaiwa kwamba kati ya 2020 na Januari 2023 ndipo alipotekeleza matukio hayo kwa kumbaka binti (9) kosa ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na 131 (1) (3) na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) na (2) vyote vya sura ya 16 vilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022. 

Baada ya kuridhika na ushahidi huo wa upande wa Serikali na mshtakiwa kutokuwa na cha kujitetea Hakimu mfawidhi mkoa wa Mbeya Zawadi David Laizer amemhukumu Ezekia Msawile kwenda jela maisha kwa kosa la kwanza na kwa kosa la pili amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na adhabu zote hizo zimeelekezwa kwenda kwa pamoja hivyo mtu huyo atatumikia kifungo cha maisha jela na upande usioridhika na hukumu hiyo una haki ya kukata rufaa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted