Chadema yalimwa barua na Msajili wa Vyama vya Siasa, awataka wajieleze  kuhusu kuchapisha maudhui yanayomdhalilisha mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu

Chama cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA, kimesema kimepokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania ikiwataka wajieleze kuhusu kutengeneza maudhui yanayotajwa kuwa yanamdhalilisha Mwenyekiti wa CCM...

0

Chama cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA, kimesema kimepokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania ikiwataka wajieleze kuhusu kutengeneza maudhui yanayotajwa kuwa yanamdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassani.

Kupitia ukuarasa wake wa X Katibu Mkuu wa CHADEMA ndugu John Mnyika ameeleza kuwa video hiyo wanayodaiwa kuitengeneza inajulikana kama “2025 Tuagane CCM “ ambayo Chama cha Mapinduzi waliwasilisha malalamiko wakidai inaashiria kuwa bango hilo limetengenezwa na kusambazwa kwenye mitandao ya CHADEMA au wafuasi wake.

“Nawataarifu wanaChadema kuwa tumepokea barua ya Msajili wa Vyama ya kutaka Chadema, tujieleze ndani ya siku 5 juu ya video ya “2025 Tuagane CCM ” ambayo Chama cha Mapinduzi,wamewasilisha malalamiko kuwa imedhalilisha Mwenyekiti wa Chama hicho. CCM wamedai kuwa maudhui ya video hiyo “yanaashiria kuwa bango hilo limetengenezwa na na kusambazwa kwenye mitandao na Chadema au wafuasi wake”. ameandika Mnyika kupitia ukurasa wake wa X

Kwa mujibu wa Mnyika ni kwamba walipokea barua hiyo Oktoba 2,2023 hata hivyo baada ya kupitia mitandao yao ya CHADEMA bado hakufanikiwa kuiona video yenye maudhui hayo yanayolalamikiwa na CCM, na kwamba CHADEMA haijaandika wala kuchapisha video yenye maudhui yanayolalamikiwa.

 “Toka nilipopokea barua hiyo tarehe 2 Oktoba 2023 nimepitia mitandao rasmi ya kijamii ya Chadema sijaona video hiyo. Nafahamu pia kwamba Chadema haijatengeneza video yenye maudhui kama hayo yanayolalamikiwa. Hata hivyo, kwa kuwa katika malalamiko hayo Msajili na CCM wamehusisha pia “wafuasi wa Chadema”. Nawaandikia ujumbe huu wa wazi ili mfahamu juu ya malalamiko hayo”

Aidha Mnyika amewaomba wanachamana na wafuasi wa CHADEMA, ikiwa kuna yoyote mwenye rejea juu ya chochote kilichosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM au wafuasi wake chenye kudhalilisha Chadema au viongozi wake akiweke au akiwasilishe kwake kwa ajili ya Msajili wa Vyama kuwaandikia CCM nao kuwasilisha maelezo. 

Amedai kuwa hayo yanayotokea hivi sasa kwenye ofisi ya Msajili yametokana na uwepo wa kanuni kandamizi zilizotokana na marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya 2019, huku akisisitiza umuhimu na haja ya kupatikana kwa mabadiliko ya Katiba Mpya.
“Ni vyema ijulikane kuwa Msajili amepata mamlaka haya kutoka katika kanuni kandamizi za Maadili ya Vyama Vya Siasa za mwaka 2019 zilizotokana na marekebisho mabaya ya Sheria ya Vyama Vya Siasa ya 2019. Hivyo, tuendelee kutaka Katiba Mpya itayowezesha kuwa na taasisi huru ikiwemo ofisi huru ya Msajili wa Vyama na kutungwa kwa sheria mpya ya Vyama itakayolinda demokrasia , uhuru na haki za vyama Vyama Vya Siasa” amesema Mnyika.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted