CCM yamteua Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake

Dk Nchimbi anachukua nafasi ya Daniel Chongolo ambaye alijiuzulu kwa kile alichodai kuwa amechafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

0

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho.

Dk Nchimbi anachukua nafasi ya Daniel Chongolo ambaye alijiuzulu kwa kile alichodai kuwa amechafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Uteuzi wa Dk Nchimbi umefanyika leo Jumatatu Januari 15, 2024 wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Samia Suluhu, kisha kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyofanyika mjini Unguja, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo Dk Nchimbi aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri kabla ya kumaliza muda wake. Awali alikuwa mbunge wa Songea mjini (CCM) kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 pia alikuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted