Watu 17 wameokolewa kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV MAMAN BENITA

Taarifa ya TASAC imeeleza kuwa baada ya kuzama Aprili 7, 2024, Wavuvi walimuokoa Abiria mmoja raia wa China na hadi Saa 1:00 Usiku wa Aprili 7, 2024, Watu...

0

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema Watu 17 wameokolewa katika tukio la kuzama kwa Meli ya MV Maman Benita iliyokuwa inatoka Kigoma kuelekea Kalemie nchini Congo katika Ziwa Tanganyika ikiwa na Abiria 27, Aprili 6, 2024.

Taarifa ya TASAC imeeleza kuwa baada ya kuzama Aprili 7, 2024, Wavuvi walimuokoa Abiria mmoja raia wa China na hadi Saa 1:00 Usiku wa Aprili 7, 2024, Watu 17 waliokolewa ambapo Wachina 2, Watanzania 3 na Wakongo 12. 

Chanzo cha kuzama kwa meli hiyo bado hakijajulikana huku Nahodha akiwa ni kati ya waliookolewa.

 Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa meli hiyo iliyozama eneo la Kabimba, DRC iliyosajiliwa chini ya Bendera ya DRC na inamilikiwa na kampuni ya Kikongo, iitwayo Établissement Manimani, ilikuwa na Raia wa Tanzania (5), China (4), DRC (16), Kenya (1) na mtoto mdogo.

TASAC inaendelea kutoa rai kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo majini kuzingatia Sheria na Kanuni za udhibiti usafiri majini na kuhakikisha chombo kina kuwa na majaketi okozi ya kutosha na kwa vyombo vidogo kuhakikisha abiria wanavaa jaketi okozi wakati wote wa safari ili kujiepusha na maafa yanayoweza kusababishwa na tukio la ajali.

Aidha, TASAC inatoa pole kwa waathirika pamoja na familia kwa ujumla na taarifa kamili juu ya ajali hii itatolewa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted