Dereva wa basi la shule lililosombwa na maji na kuua wanafunzi saba Arusha ashtakiwa kwa kuua bila kukusudiwa.

Dereva huyo anayefahamika kwa majina ya Lukuman Hemed amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Sheila Mameto huku kesi hiyo...

0

Dereva wa basi la shule ya msingi Ghati  Memorial lililosomwa na maji na kuua wanafunzi saba jijini Arusha amepandishwa kizimbani na kusomewa  mashtaka nane likiwemo la kuua bila kukusudia.

Dereva huyo anayefahamika kwa majina ya Lukuman Hemed amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Sheila Mameto huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Aprili 30 mwaka huu, baada ya Mawakili wa upande wa Jamhuri kusema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Itakumbukwa kuwa ajali hiyo ilitokea Aprili 12,2024 alfajiri baada ya gari hilo lilokuwa na watu 13 kutumbukia kwenye korongo na kusababisha wanafunzi hao kufariki baada ya kusombwa na maji.

Aidha dhamana ya dereva huyo imepingwa na mawakili wa Jamhuri kwa kile kilichodaiwa kuwa usalama wake uko hatarini kutokana na wananchi kuwa na hasira na dereva huyo aliyesababisha ajali licha ya kuchwa Hakimu alitangaza kuwa nafasi ya dhamana iko wazi.

Hata hivyo mshtakiwa alipoulizwa juu ya pingamizi hilo alikubaliana nalo na hivyo kupelekwa katika gereza la kisongo hadi Aprili 30,2024

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted