‘Walipe kama unataka!’ Ruto awaambia wanaounga mgomo wa madaktari

Madaktari madkatrai nchini Kenya wametishia kuacha kufanya uchunguzi wa maiti na kujaza kujaza fomu za P3 iwapo polisi watahujumu na kuwazuia kufanya maandamano yao.

0
(Photo by SIMON MAINA / AFP)

Madaktari madkatrai nchini Kenya wametishia kuacha kufanya uchunguzi wa maiti na kujaza kujaza fomu za P3 iwapo polisi watahujumu na kuwazuia kufanya maandamano yao. Pia wamesema wamewacha kulekea kortini kutoa ushihuda kwa niaba ya polisi.

Haya yanajiri wakati Mgomo ukichukua sura mpya baada ya magavana kutishia kuwachukulia hatua za sheria ya ajira, huku tume ya haki za binadamu ikitoa wito madaktari kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Madaktari na matabibu Walimiminika barabarani kwa maandamano guu kwa guu jijini Nairobi hadi ofisi za baraza la magavana. Madaktari hao wametoa ilani ya kuandamana kila Jumanne hadi pale kilio chao kitakaposikilizwa.

Kwa upande wake, waziri wa afya wa Kenya, Susan Nakhumicha anasisitiza kuwa wanafanya kila lililo ndani ya uwezo wao kufikia mwafaka.

Wizara ya afya ya Kenya imependekeza madaktari wanafunzi kupewa shilingi alfu 70 za Kenya wanaponoa ujuzi wao kwenye hospitali za umma. Mpango huo utaigharimu serikali shilingi bilioni 2.4.

Licha ya hayo, Rais William Ruto ameweka bayana wazi kuwa serikali haitawapa madaktari nyongeza ya misharara liwe liwo

"Tuna changamoto ya madaktari. Tuna viongozi wakiwemo magavana wanaosema 'Tunaunga mkono mgomo wa madaktari'. Kweli?" "Ikiwa unaunga mkono mgomo wao basi ulipe pesa wanazoomba."Alisema Ruto

Hata hivyo, madaktari wenyewe kupitia Chama chao cha KMPDU wanadai walipwe shilingi laki mbili za Kenya kiasi ambacho ni maradufu ya kile kinachopangwa na serikali.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted