Kesi ya Lissu: Shahidi Akiri Kutoeleza Tofauti ya Ushahidi wa Maelezo ya Polisi na Aliotoa Mahakamani
Lissu: Shahidi, nataka kwanza nianze na maswali yangu ya jana kuhusu tofauti kati ya ushahidi ulioutoa kwenye maelezo ya polisi na ushahidi ulioutoa kizimbani. Waeleze Waheshimiwa Majaji kama unaamini maelezo yako yanapaswa kuaminiwa na mahakama.
Shahidi: Ni kweli.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kuna mahali umeeleza sababu za tofauti kati ya ulichoandika na ulichosema mahakamani.
Shahidi: Hakuna mahali.