Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki dunia. - Mwanzo TV

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki dunia.

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga.

Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

“Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua,” amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

“Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia,” amesema Balozi Sokoine.