Mawaziri SADC wajadili hali ya amani DRC na Msumbiji
Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Nandi Ndaitwah ambapo pamoja na mambo mengine, amezisihi Nchi wanachama wa SADC kuendelea kushirikiana na DRC pamoja na Msumbiji na kuhakikisha kuwa hali ya amani inarejea.