Tanzania yakanusha uwepo wa mwekezaji aliyepewa bandari ya Bagamoyo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa Tanzania imesaini mkataba wa kuipa Kampuni ya Saudi-Africa Development Company (SADC) haki ya kuendesha Bandari ya Bagamoyo.