Waziri Mkuu wa DRC asema zaidi ya watu 7,000 wamefariki mashariki mwa nchi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) alisema Jumatatu kwamba zaidi ya watu 7,000 wamefariki mashariki mwa nchi hiyo tangu mwezi Januari, wakati kundi la M23 lililokuwa likiungwa mkono na Rwanda lilipochukua miji miwili mikubwa.