Mtu mmoja afariki dunia huku wengine saba wakijeruhiwa kwa mlipuko wa baruti
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa amesema aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni Marco Msenyere (52), mpasua mawe na mkazi wa Semba-Lwanhima. Wakati wa tukio hilo, marehemu alikuwa na wenzake wakinywa kahawa kwenye kibanda hicho akiwa na begi dogo ambalo ndani yake lilikuwa na baruti hizo.