Wafuasi wa Chadema Mwanza wapigwa marufuku kufanya mikusanyiko kesho Lissu akifikishwa mahakamani
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limetoa tahadhari kwa wananchi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaopanga kufanya mikusanyiko na maandamano ya kuishinikiza Serikali kuachiwa huru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ambaye kesho Aprili 24,2025 atafikishwa mahakamani.