Wasichana Milioni 79 kusini mwa Sahara wamekumbana na ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia:UNICEF
Duniani kote, UNICEF inakadiria kwamba unyanyasaji wa kijinsia umewakumba wasichana na wanawake wapatao milioni 370, huku takriban mmoja kati ya watano aliyopo Kusini mwa Sahara akipitia unyanyasaji wa kijinsia au ubakaji kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.