Msako Mkubwa Wafanywa Syria katika jela la Saydnaya Linaloaminika Kuwa “Kichinjio Cha Binadamu”
Wafungwa waliokuwa wakishikiliwa ndani ya jengo hilo, ambalo lilikuwa eneo la kunyongwa bila ya mahakama, kuteswa na kutoweka kwa lazima, waliachiliwa mapema wiki iliyopita na waasi waliomtimua kiongozi wa Syria Bashar al-Assad mnamo Desemba 8, 2024.