Mahakama Kuu kusikiliza maombi ya Habeas Corpus ya John Heche
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi, maombi hayo yamesajiliwa na kupangwa mbele ya Jaji Obadia Bwegoge.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi, maombi hayo yamesajiliwa na kupangwa mbele ya Jaji Obadia Bwegoge.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema kuwa baadhi ya taarifa hizo zimeandaliwa kwa uangalifu ili kuzalisha taharuki, ikiwemo kuchukua matukio yaliyotokea katika nchi nyingine, kuyatengeneza upya, kisha kuyaunganisha na sauti za Kiswahili zenye lafudhi ya nchi yetu ili yaonekane yametokea nchini.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imewahukumu vijana wanne kifungo cha miaka saba jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kumteka mfanyabiashara Deogratus Tarimo.
Kati ya Januari 2024 na Oktoba 2025, Amnesty iliripoti ukiukaji mpana wa haki za binadamu ikiwemo matukio ya watu kupotea kusikojulikana, mateso na mauaji ya kiholela ya viongozi na wanaharakati wa upinzani.
Lissu, ambaye anajitetea mwenyewe, anakabiliwa na shtaka la uhaini yanayodaiwa kutokana na matamshi aliyotoa Aprili 3,2025. Alikamatwa Aprili 9, 2025 mkoani Ruvuma na kisha kusafirishwa hadi Dar es Salaam, ambako anakabiliwa na kesi hiyo mbele ya jopo la majaji wa Mahakama Kuu.
Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Lissu aliendelea na zoezi la kumhoji kwa kina shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka, akichambua maelezo yake ya polisi dhidi ya ushahidi alioutoa mahakamani wiki iliyopita.
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeridhia maombi ya mawakili wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kuwasilisha kiapo cha ziada katika shauri la maombi ya kutekwa kwa utaratibu wa kisheria (Habeas Corpus).
Shahidi wa kwanza alihitimisha ushahidi wake leo baada ya kuhojiwa kwa maswali ya nyongeza na jopo la mawakili wa Serikali
Katika mahojiano hayo, Lissu alitumia takribani saa saba kumuhoji Shahidi huyo kuanzia majira ya saa 3:30 mpaka saa 10, muda wote aliutumia kupima uhalali wa ushahidi wa shahidi huyo, akihusisha masuala mbalimbali kulinga na ushahidi aliouandika katika maelezo yake ikiwamo ya taratibu za kiuchunguzi, matumizi ya notebook ya polisi, video za ushahidi na tafsiri ya maneno yaliyotumika kwenye mashtaka ya uhaini.
Akijibu ripoti iliyotolewa na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Human Rights Watch (HRW), Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema madai hayo hayana msingi na yanapotosha hali halisi ya nchi.