Marais Samia na Hichilema wahudhuria mkutano wa UN kwa mara ya kwanza

Zaidi ya viongozi 100 na wakuu wa serikali wanakutana katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini...

0

Zaidi ya viongozi 100 na wakuu wa serikali wanakutana katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Newyork. Mkutano huu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulianza Jumatatu 20 Septemba kwa burudani kutoka kwa kikundi cha wasanii BTS kutoka Korea Kusini.

BTS, Wasaanii wa Korea Kusini

Mijadala ilianza Jumanne na itaendelea kwa siku tisa na kuwapa fursa viongozi tofauti kuhutubia jamii ya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na maafisa wengine wanaendeleza msukumo wa kuwashawishi washiriki juu ya umuhimu wa shirika la Umoja wa Mataifa wakati dunia kwa jumla ikipambana na janga la UVIKO 19 na mabadiliko ya tabianchi.

Shida tulizozisababisha ni shida ambazo tunaweza kuzitatua. Ubinadamu umeonyesha kuwa tunauwezo wa kufanya mambo makubwa ikiwa tutafanya kazi pamoja. Antonio Guterres, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa.

Kati ya viongozi wanaohudhuria mkutano huu wa UNGA kwa mara ya kwanza ni Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kutoa hotuba yake Alhamisi, Septemba 23.

Kuhudhuria kwa mkutano huu wa wa kimataifa wa UNGA kwa rais wa Tanzania unonesha mabadiliko ya sera ya mambo ya nchi za nje kwa rais huyu mpya ikilinganishwa na miaka takriban 6 ya Rais John Magufuli ambaye katika muda ambao alikuwa rais wa Tanzania hakuwahi kuhudhuria mikutano yoyote ya kimataifa wala ya kanda ya Afrika.

Uamuzi wa Rais Samia Suluhu kuhudhuria kikao hiki cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini Newyork ni moja ya maazimio yake ya kuweka mabadiliko katika sera za kimataifa. Azimio lake la kukutana ana kwa ana na viongozi wengine wa mataifa ya nje ni katika juhudi zake za kujenga ushirikiano na mataifa mengine ambao ulisambaratika wakati wa uongozi wa takriban miaka sita wa mwandazake Rais John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema atakuwa anahutubia kikao hicho Alhamis 22. Kati ya masuala ambayo Rais Hichilema anatarajiwa kuzungumzia ni maendeleo ya kiuchumi, ajira, fursa za biashara, elimu na huduma bora za afya kwa watu wa Zambia.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuhusu Zambia kuwa demokrasia inapatikana katika vijana wa Zambia, alwapongeza vijana wa Zambia kwa kujitokeza kwa wingi na kupiga kura ambayo ilileta mabadiliko ya uongozi katika taifa hilo.

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema

Katika mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Biden aliwataka viongozi wa mataifa yote duniani kupigania haki za wanawake na makundi ya LGBTQ katika mataifa yao.

“Maisha bora ya baadaye yatakuwa ya wale wanaokumbatia utu na sio kuuangamiza.’ Rais Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted