Mfahamu mwanamke wa kwanza mwafrika aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel

Mwaka wa 2004 Wangari Maathai alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mchango wake katika maendeleo endelevu, demokrasia na amani.Maathai alikuwa mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda tuzo hiyo

0
Wangari Maathai

Septemba 25 mwaka 2011 mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel, Wangari Maathai alipaga dunia akiwa na umri wa miaka 71.

Wangari Muta Maathai alizaliwa 1 Aprili mwaka 1940, na alikuwa mwanaharakati wa kijamii, mazingira, na kisiasa. Wangari Maathai alisomea nchini Marekani baada ya kushirikishwa kwa mpango wa “The Kennedy Airlift,” mpango uliowapa Waafrika nafasi ya kusomea nchini Marekani. Alifuzu na shahada ya kutoka chuo kikuu cha Mount St.Scholastica na shahada ya uzamili kutoka chuo cha University of Pittsburgh. Wangari Maathai alikuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika mashariki na kati kuwa Daktari wa Falsafa baada ya kupokea shahada ya falsafa kutoka chuo kikuu cha Nairobi, Kenya.

Mwaka wa 1977, Wangari Maathai alianzisha Green Belt Movement kama shirika lisilo la kiserikali la mazingira, shirika hilo lilijihusiha na upandaji wa miti,utunzaji wa mazingira na kupigania haki za wanawake.

Maathai alihudumu kama mbunge kati ya Januari 2003 na Novemba 2005 na pia Naibu Waziri wa Mazingira na Raslimali katika serikali ya rais wa tatu wa Kenya, Mwai Kibaki.

Juhudi zake za kutunza mazingira nchini Kenya zilimletea maadui wengi, hususan kutoka kwa viongozi wa kisiasa. Mwaka wa 1989, Maathai aligundua kuhusu mpango wa kujengwa kwa jengo la ghorofa 60, jengo hilo la Kenya Times Media Complex lilikulijengwe katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi na kutumiwa kama makao makuu ya chama cha KANU kilichokuwa uongozini wakati huo.

Ili kupinga ujenzi huo, Maathai aliandika barua nyingi kupinga ujenzi huo, aliandikia barua kwa gazeti la Kenya Times,kwa Ofisi ya Rais, kwa tume ya jiji la Nairobi, kwa Waziri wa Mazingira na Raslimali, kwa wakurugenzi wa Shirika la Mazingira la UNEP na hata kwa Balozi wa Uingereza,Kenya Sir John Johnson.

Licha ya kuandika barua nyingi na kupinga ujenzi huo, shughuli za ujenzi zilianza 15 Novemba 1989. Maathai alitafuta zuio katika Mahakama Kuu ya Kenya kusitisha ujenzi, lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali 11 Desemba.Ujenzi huo ulisitishwa baada ya wawekezaji wa kigeni kughairi mradi huo mnamo Januari 1990.

Miaka kadhaa baadae 2022, Wangari Maathai aliwania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Tetu, alishinda uchaguzi huo kwa tiketi ya chama cha National Rainbow Coalition na Januari 2023 akateuliwa kwa nafasi ya naibu Waziri wa Mazingira na Raslimali.

Mwaka wa 2004 Wangari Maathai alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mchango wake katika maendeleo endelevu, demokrasia na amani.Maathai alikuwa mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda tuzo hiyo.

“Maathai alisimama kwa ujasiri dhidi ya utawala wa zamani wa kidhalimu nchini Kenya. Amepigania wengi kupata haki za kidemokrasia na haswa amehimiza wanawake kuboresha hali zao.” Taarifa yaThe Norwegian Nobel Committee, walipomtangaza kama mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2004.

Wangari Maathai

Mnamo Agosti 2006, aliyekuwa seneta wa jimbo la Chicago Barack Obama alizuru Kenya, yeye na Maathai walipanda mti pamoja katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na Wangari Maathai

Kwa kumbukumbu na heshima ya Wangari Maathai, bustani ya Wangari Gardens ilifunguliwa rasmi mjini Washington DC, Marekani.

Mwaka wa 2014, chuo cha Mount St. Scholastica nchini Marekani alikosomea kilizindua sanamu kwa heshima ya kazi yake katika uhifadhi wa mazingira.

Sanamu ya Wangari Maathai

Oktoba 2016, barabara ya Forest Road mjini Nairobi ilibadilishwa jina na kuitwa Wangarĩ Maathai Road kwa heshima yake na juhudi zake za kutunza misitu kupitia shirika lake la Green Belt Movement.

Wangari Maathai aliaga dunia baada ya kuugua saratani 25 Septemba 2011.

Angalia video ya maisha yake kupitia Shangazi Power hapa:

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted