Maafisa saba wa UN wafukuzwa kutoka Ethiopia.

Ethiopia imewafukuza maafisa saba wa Umoja wa Mataifa UN ambao walituhumu kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi.

0

Ethiopia imewafukuza maafisa saba wa Umoja wa Mataifa ambao walituhumu kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi,wakati shinikizo likiendelea kukua kuhusu  kizuizi kilichowekwa kwa mkoa wa Tigray.

Hatua ya kuwafukuza maafisa hao ilikuja baada ya serikali ya Ethiopia kuweka vizuizi vya misaada kufikia takriban watu milioni 6 katika mkoa wa Tigray baada ya kipindi cha mwaka mmoja wa mapigano.

Shirika la Umoja wa Mataifa limekuwa likizungumzia wazi uamuzi wa serikali ya Ethiopia kuzuia misaada ya chakula,vifaa vya matibabu na mafuta ambavyo vimezuiwa kuwafikia watu katika mkoa wa Tigray kwa wiki kadhaa sasa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imesema maafisa hao wanapaswa kuondoka Ethiopia ndani ya saa 72. Maafisa hao wanajumuisha maafisa watano kutoka Shirikla la watoto la UNICEF na wengine wawili wa Shirika la kutetea haki za binadamu la UN.

Majeshi ya serikali yamekuwa yakipigana na majeshi ya Tigray ya TPLF ambayo yamekuwa yakidhibiti eneo la Tigray kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni mbili wametoroka makaazi yao.

Abiy Ahmed, Waziri Mkuu Ethiopia
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted