Elon Musk na Jeff Bezos kando, tajiri mkubwa zaidi alikuwa mwafrika

Kulingana na wanahistoria, Mansa Musa bado ndio mtu tajiri zaidi aliyewahi kuishi,thamani yake kwa viwango vya fedha vya sasa ni dola bilioni 400.

0
Mansa Musa mfalme wa himaya ya Mali

Baada ya kulipuka kwa UVIKO 19 takriban miezi 22 iliyopita uchumi wa mataifa mengi ulizorota huku watu wengi wakipoteza kazi zao.

Ingawaje watu wengi walipoteza ajira na mataifa kushuhudia mfumuko wa bei za bidhaa, kuna takriban watu watano ambao walitajirika zaidi katika kipindi cha UVIKO 19.

Kufikia 2021, idadi ya mabilionea iliongezeka na kufika 2,755 huku utajiri wa mabilionea Jeff Bezos, Elon Musk, Bill Gates, Mark Zuckerberg, Larry Page na wengine uliongezeka kwa 62% katika kipindi cha UVIKO 19.

Mtu tajiri zaidi duniani katika historia ya sasa ni bilionea Elon Musk. Musk ni Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Tesla na mwanzilishi wa SpaceX na The Boring Company.Thamani yake inakadiriwa kuwa dola bilioni 288 bilioni.

Katika habari za hivi karibuni, Elon Musk alipoteza kiasi cha dola bilioni 50 ndani ya saa 48 baada ya mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter kumtaka auze hisa zake katika kampuni ya Tesla ili asaidie mataifa maskini duniani. Hata baada ya kupoteza mamilioni yote hayo ndani ya saa 48 bado ndiye mtu tajiri zaidi duniani.

Elon Musk, mtu tajiri zaidi duniani na mmiliki wa Tesla


Elon Reeve Musk alizaliwa na kulelewa Afrika Kusini katika mji mkuu wa Pretoria kabla kuhamia nchini Amerika alikopata elimu yake ya chuo kikuu.

Mtu anayeshikilia nafasi ya pili kwa utajiri ni Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon na mmiliki wa Blue Origin, anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 201.Utajiri wake uliongezeka kwa $24 bilioni katika kipindi cha UVIKO 19.

Elon Musk, Jeff Bezos na hata Bill Gates ni mabilionea ambao wamefahamika sana duniani kwa utajiri wao. Lakini je wajua kuwa mtu tajiri zaidi kuwahi kuishi alikuwa na utajiri mkubwa zaidi kumliko Elon Musk na alikuwa mwafrika.

Mansa Musa kutoka Afrika anasemekana kuwa mtu tajiri zaidi duniani hata katika viwango vya sasa.

Kulingana na wanahistoria, Mansa Musa bado ndio mtu tajiri zaidi kuwahi kuishi.Hata baada ya kukadiria utajiri wake kulingana na mfumuko wa bei wa sasa,thamani yake ni dola bilioni 400.

Musa alizaliwa mwaka wa 1280, jina Mansa linamaana ya ‘Sultan’ kwa lugha ya Mandika. Musa alikuja madarakani mwaka wa 1312 na kuongoza himaya hiyo kwa miaka 25. Himaya ya Mali ilijumuisha nchi za Senegal, Mali, Burkina Faso, Niger, Guinea na Ivory Coast. 

Mansa Musa mfalme wa Mali

Ingawaje himaya hiyo ilikuwa tajiri kabla aingie madarakani, uongozi wake ulileta utajiri na mafanikio zaidi, utajiri ukitokana na dhahabu na chumvi iliyopatikana kwa wingi magharibi mwa Afrika.

Kando na kuwa mfalme wa himaya ya Mali, alikuwa pia sultan na alishikilia dini kama kiongozi wa kiislamu. Musa alitimiza guzo tano za dini ya kiislamu, ikiwemo kuenda Hajj. Katika safari moja wapo za kuenda Hajj, Mansa Musa aliamua kuzuru Misri akielekea Saudia Arabia.

Katika ziara hiyo, Musa aliyefahamika kama mfalme wa wafalme alipeana dhahabu nyingi kwa maskini katika nchi ya Misri hadi bei na thamani ya dhahabu ikadorora kwa miaka kumi na miwili pamoja na uchumi wa Misri kuporomoka.

Safari ya Mansa Musa ya kuenda Hajj mwaka wa 1324 ilijumuisha watumishi 13,000 na shehena 100 za ngamia za dhahabu safi.

Musa alisifika kwa ukarimu na uchamungu wake, alijenga msikiti kila Ijumaa katika safari zake na alipeana dhahabu nyingi kiasi kwamba iliyumbisha uchumi katika sehemu za eneo hilo kwa miaka kumi na miwili – pamoja na kudhoofisha thamani ya dhahabu. Mansa Musa litumia utajiri wake mkubwa kujenga msikiti kila mwaka, alijenga vyuo vikuu na shule ikiwemo maktaba kubwa na kongwe zaidi duniani.Utawala wake unahusishwa na miradi mingi ya ujenzi, pamoja na ujenzi wa Msikiti wa Djinguereber huko Timbuktu ulioko hadi sasa.

Msikiti wa Djinguereber mjini Timbuktu

Majengo mengi aliyoyajenga katika kipindi cha miaka 20 ya uongozi wake bado yapo hadi sasa katika mji wa Timbuktu.

Hija yake, ukarimu na sifa yake ulitambulisha ulimwengu kuhusu utajiri mkubwa wa Afrika, na haswa, Mali.

Mansa Musa mfalme wa Himaya ya Mali
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted