Wanafunzi wa Korea Kusini waandika mtihani mgumu zaidi duniani

Maisha ya wanafunzi hutegemea sana alama watakazopata katika mtihani huu wa Suneung kutoka chuo kikuu watakachosomea, hadi kazi watakazofanya, mshahara watakaopokea na hata uhusiano wa kimapenzi wa baadae

0
Wanafunzi wa Korea Kusini wakiandika mtihani wa Suneung


Tarehe 18 Novemba kila mwaka, Korea Kusini hugubikwa na utulivu wa ajabu wakati takriban wanafunzi milioni moja wanapoandika mtihani muhimu sana na ambao sehemu kubwa ya maisha yao itategemea,mtihani huo unajulikana kama Suneung.

Sio tu kwamba mtihani huo umehusishwa na matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana, wakosoaji wanasema unalenga sana kujifunza kwa kukariri na unahitaji kufanyiwa utafiti upya.

Kila mwaka wakati kama huu, wazazi na mababu hutembelea hekalu la kihistoria la Jogyesa ili kuwaombea watoto na wajukuu zao ambao watakuwa wakifanya mtihani wa Suneung ambao utawawezesha kujiunga na vyuo vikuu.

Wazazi wakiwaombea watoto wao katika hekalu la Jogyesa

Mtihani hudumu kwa saa nane, wanafunzi hupewa alama kati ya 1 hadi 9 kulingana na ulivyofanya kwenye somo fulani, alama ya 9 ikiwa ya juu zaidi. Kati ya masomo wanayofanyia mtihani ni Kikorea, hisabati, Kiingereza, historia ya Kikorea na masomo ya chini ya sayansi ya jamii, sayansi, masomo ya ufundi na lugha ya pili ya kigeni au herufi za Kichina.

Maisha ya wanafunzi hutegemea sana alama watakazopata katika mtihani huu wa Suneung kutoka chuo kikuu watakachosomea, hadi kazi watakazofanya, mshahara watakaopokea na hata uhusiano wa kimapenzi wa baadae.

Katika siku ya mtihani Novemba 18,  ili kuzuia usumbufu kwa wale wanaoandika mtihani, ufunguzi wa masoko ya hisa hucheleweshwa saa moja, ndege zinazoingia nchini hubadili ratiba zao ili kuepuka kutua wakati wa vipindi muhimu vya mtihani, serikali huboresha huduma za uchukuzi wa umma ili kuzuia msongamano wa magari na maafisa wa polisi wamejulikana kuwasindikiza wanaofanya mtihani ili wasichelewe.

Mtihani wa Suneung umekuwa kama ibada kwa vijana wa Korea Kusini tangu ulipoanzishwa mwaka wa 1994, lakini wasiwasi unazidi kutanda juu ya umuhimu wake katika kuandaa akili za vijana kwa siku zijazo.

Wakosoaji wanasema mtihani huo umekuwa kwa kiasi kikubwa mtihani wa matajiri, ikiwa kama kipimo cha wazazi ambao wanaweza kumudu kuwapeleka watoto wao katika shule bora zaidi. Wakosoaji pia wanahoji msisitizo wake juu ya kujifunza kwa kukariri kwa gharama ya ubunifu.

Wengi sasa wanadai mfumo wa kutoa alama urekebishwe ili kuhimiza mtazamo kamili zaidi wa kujifunza na kupunguza shinikizo kwa vijana.

“Matokeo ya mtihani wa Suneung yote yanategemea ni kiasi gani cha elimu ya kibinafsi ambacho mwanafunzi amepokea,” alisema Lee Yoon-kyoung, mkurugenzi wa Chama cha Kitaifa cha Wazazi cha Elimu ya Cham.

“Huwezi kusomea mtihani wa Suneung shuleni, lazima usomee katika shule maalum ya kukariri.”

Alieleza kuwa wakati shule zilijikita katika kufuata mtaala uliowekwa na serikali, maswali ya mtihani wa Suneung yalitungwa tofauti na mara zote hayaakisi mtaala.

Kwa hivyo, ni kawaida kwa wanafunzi kuzingatia zaidi vitabu vya kibinafsi vya kusoma vilivyobobea katika Suneung ambavyo vinatengenezwa na Mfumo wa Utangazaji wa Kielimu wa Korea.

Wanafunzi wa darasa la 12, ikiwa ndio mwaka wa mwisho kabla kujiunga na chuo kikuu hutafuta visingizio vya kukosa masomo ili waweze kutumia wakati mwingi katika shule za cram na masomo ya kibinafsi.Kumekuwa na ripoti za wanafunzi kuacha shule ili kujiandaa vyema kwa mtihani huo.

Wanafunzi wakitoka darasani baada ya kuandika mtihani wa Suneung

Shinikizo kubwa kwa wanafunzi kufanya vyema katika mtihani wa Suneung ni kwa sababu bila alama nzuri wanafunzi hukosa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu bora zaidi ambavyo vitawahakikishia kupata ajira katika mashirika makubwa, ambayo kwa Wakorea Kusini wengi ndio lengo kuu.

Asilimia 2 pekee ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa Senueng hufaulu kujiunga na vyuo vitatu bora zaidi nchini Korea Kusini.

Mtazamo wa mfumo wa elimu unaohitaji wanafunzi kupata alama za juu mara nyingi hutajwa kama sababu ya matatizo ya afya ya akili yanayowakabili vijana.

Korea Kusini ina kiwango cha juu zaidi cha watu wanaojiua kati ya mataifa ya kiuchumi ya OECD.Na ingawa katika miaka ya hivi majuzi kiwango hicho kimepungua kwa takriban vikundi vyote vya umri kati ya 30 na 80, watu wanaojiua miongoni mwa watu wenye umri wa miaka tisa hadi 24 wamekuwa wakiongezeka kwa kasi. Mnamo 2019, kikundi hiki kilijumuisha watu 876 waliojiua, au watu 9.9 waliojiua kwa kila vijana 100,000.

Katika baadhi ya vifo, mtihani wa Suneung umetajwa kuwa sababu ya moja kwa moja.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted