Rwanda Kuajiri Zaidi ya Walimu 300 kutoka Zimbabwe

Hatua hiyo inakuja miezi miwili tu baada ya Rais Paul Kagame kutoa ombi hilo wakati wa mkutano wa biashara na uwekezaji wa nchi hizo mbili.

0

Rwanda na Zimbabwe zimetia saini mkataba wa makubaliano utakaoruhusu Kigali kuajiri walimu kutoka Zimbabwe ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo inakuja miezi miwili tu baada ya Rais Paul Kagame kutoa ombi hilo wakati wa mkutano wa biashara na uwekezaji wa nchi hizo mbili.

Takwimu za Wizara ya Elimu zinaeleza kuwa walimu hao 273 wa Mafunzo ya Ufundi pamoja na 33 ambao watapangiwa Vyuo vya Ualimu.

Chini ya makubaliano hayo, walimu watatoa masomo katika shule shirikishi za uuguzi na chuo cha dawa na sayansi ya afya, wizara ya Rwanda ilisema.

Waziri wa Utumishi wa Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Zimbabwe Paul Mavima alisema makubaliano hayo yana kanuni zinazokuza “kanuni za kazi zenye staha katika mchakato mzima wa kubadilishana wafanyakazi na utaalamu, ikiwa ni pamoja na masuala muhimu katika uhamaji wa wafanyikazi kama vile kutobaguliwa.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted