Mbowe kuongoza kikao cha kamati kuu CHADEMA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, kupitia ukurasa wake wa Twitter ni kwamba maamuzi ya chama kutokana na ajenda mbalimbali zitakazojadiliwa yatatolewa...

0
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe anatarajiwa kuongoza kikao cha kamati kuu ya chama hicho tarehe 16 Machi 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, kupitia ukurasa wake wa Twitter ni kwamba maamuzi ya chama kutokana na ajenda mbalimbali zitakazojadiliwa yatatolewa baada ya kikao hicho.

Mbowe ataongoza kikao hicho ikiwa ni takribani zaidi ya siku 10 tangu aachiliwe huru na wenzake watatu, kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania kufuwafutia kesi ya ugaidi iliyokuwa ikiwakabili.

Hata hivyo miongoni mwa yanayosubiriwa ni juu ya chama hicho kuwajadili wabunge 19 waliofukuzwa uanachama lakini bado wako bungeni wakidai kuwa ni wabunge wa chama hicho na bunge likibariki kuwa wanawatambua kama wanachama wa CHADEMA.

Wabunge hao 19 ni Halima Mdee, Esther Matiko,  Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, 

Wengine ni  Asia Mohammed,  Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest,  Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Novemba 27, 2020, wote kwa pamoja walivuliwa uanachama wa CHADEMA baada ya kuwa wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Swali ni je kikao hicho kitawajadili wabunge hao?

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted