Vurugu na ghasia baada ya Nigeria kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022

Ghana ilibandua nje wenyeji kwa kulazimisha sare ya 1-1 na kushinda mchezo wa hatua ya muondoano na kuondoa matumaini ya Nigeria ya kucheza Kombe la Dunia baadaye mwaka...

0

Vikosi vya usalama vya Nigeria vilirusha vitoza machozi kuwatawanya mamia ya mashabiki wenye hasira waliovamia uwanja na kufanya vurugu baada ya Nigeria kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 mwishoni mwa Jumanne.

Mashabiki waliojawa na hasira walifurika kwenye uwanja wa michezo katika mji mkuu, baada ya Ghana kuwabandua nje wenyeji kwa kulazimisha sare ya 1-1 na kushinda mchezo wa hatua ya muondoano ya Afrika kwa bao la ugenini na kuondoa matumaini ya Nigeria ya kucheza Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Baadhi ya mashabiki walivunja mabenchi huku wengine wakiimba “Pinnick lazima aondoke! Pinnick lazima aondoke!!” wakimzungumzia rais wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), Amaju Pinnick.

Mechi ya Jumanne ilikuwa mara ya kwanza tangu Oktoba 2011 kwa timu ya soka ya Nigeria kucheza katika uwanja wa MKO Abiola, ambao ulifanyiwa ukarabati wa takriban dola milioni moja ulioofadhiliwa kwa kiasi kikubwa na mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted