Mali yaanza uchunguzi kuhusu mauji yanayodaiwa kutekelezwa na Warusi

Shirika la kutetea haki za binadamu la HRW lilisema kwamba vikosi vya Mali na wapiganaji wa kigeni waliwaua raia 300 huko Moura, katika kile ilichokiita “ukatili mmoja mbaya...

0

Mali ilisema siku ya Jumatano kwamba wachunguzi wa kijeshi wameanza uchunguzi kuhusu matukio katika kijiji cha Moura, eneo la mauaji yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya ndani na wapiganaji wa kigeni.

“Kufuatia tuhuma za unyanyasaji unaodaiwa kufanywa dhidi ya raia … uchunguzi umefunguliwa na vyombo vya habari vya kitaifa kwa maagizo ya wizara ya ulinzi na askari wastaafu kufanya uchunguzi wa kina ili kutoa mwanga juu ya tuhuma hizi,” mwendesha mashtaka wa jeshi alisema katika taarifa yake.

Jeshi la Mali lilitangaza mnamo Aprili 1 kwamba limewaua wanamgambo 203 huko Moura, katikati mwa taifa hili, wakati wa operesheni mwishoni mwa Machi.

Hata hivyo, tangazo hilo lilifuatia ripoti za mitandao ya kijamii zilizosambazwa kwa wingi kuhusu mauaji ya raia katika eneo hilo.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilisema wiki hii kwamba vikosi vya Mali na wapiganaji wa kigeni waliwaua raia 300 huko Moura, katika kile ilichokiita “ukatili mmoja mbaya zaidi kuripotiwa katika mzozo wa silaha uliodumu kwa muongo mmoja nchini Mali.”

Vikosi vya Mali vilikuwa vikifanya kazi kwa pamoja na askari wa kigeni wa kizungu, kulingana na HRW, ambao wanaaminika kuwa rais wa Urusi kutokana na ripioti za mashuhuda ambazo zinawataja watu hao kutozungumza Kifaransa.

Urusi imetoa kile kinachoelezwa rasmi kama wakufunzi wa kijeshi kwa Mali.

Hata hivyo, Marekani, Ufaransa, na mataifa mengine, wanasema wakufunzi hao ni wahudumu kutoka kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Urusi ya Wagner.

Siku ya Jumatano, mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Alioune Tine alihimiza uchunguzi huru na usiopendelea upande wowote kuhusu matukio hayo.

Katika taarifa yake, alitoa wito kwa mamlaka ya Mali kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, unaojulikana kama Minusma, kufanya uchunguzi.

“Matokeo hayo lazima yawekwe hadharani na wahusika wafikishwe mahakamani,” Tine aliongeza.

Mtaalamu huyo wa haki anaungana na Marekani, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na tume ya haki za binadamu ya Mali katika kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya mauaji hayo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted