Zelensky aomba kuhutubia Umoja wa Afrika

Rais wa Ukraine,Volodymyr Zelenskyy Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameomba kuhutubia Umoja wa Afrika, Rais wa Senegal Macky Sall alisema Jumatatu. Sall, mwenyekiti wa sasa wa AU, alitweet...

0
Rais wa Ukraine,Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameomba kuhutubia Umoja wa Afrika, Rais wa Senegal Macky Sall alisema Jumatatu.

Sall, mwenyekiti wa sasa wa AU, alitweet kwamba yeye na Zelenskyy walikuwa wamejadili kwa njia ya simu athari za kiuchumi za vita vya Ukraine na “haja ya kuwa na mazungumzo kwa ajili ya kukabiliana na hatma za mzozo.”

Rais wa Ukraine pia aliomba kuhutubia AU, Sall alisema.

Ombi hilo linakuja huku kukiwa na migawanyiko ya Waafrika kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kwa mfano, nchi 58 hazikupiga kura ya Aprili 7 katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa iliyoisimamisha Urusi kutoka kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwa sababu ya uvamizi wake.

Nchi 24 za Afŕika hazikushiriki katika upigaji kura, ikiwa ni pamoja na Senegal.

Nchi nyingine tisa za Kiafrika zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo, na 9 zilipiga kura ya kulipinga.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted