Urusi: Mpango wa Uswidi na Ufini kutaka kujiunga na NATO ni ‘kosa kubwa’

Urusi ilionya Jumatatu kwamba maamuzi ya Finland na Uswidi kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO yalikuwa makosa makubwa na Moscow itachukua hatua.

0
Waziri Mkuu wa Finland Sanna Marin na Rais wa Finland Sauli Niinisto wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza kwamba Finland itaomba uanachama wa NATO katika Ikulu ya Rais huko Helsinki, Finland mnamo Mei 15, 2022 Photo by Alessandro RAMPAZZO / AFP)

Urusi ilionya Jumatatu kwamba maamuzi ya Finland na Uswidi kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO yalikuwa makosa makubwa na Moscow itachukua hatua.

“Hili ni kosa lingine kubwa lenye matokeo makubwa,”Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Ryabkov aliwaambia waandishi wa habari.

“Hali ya mivutano ya kijeshi itaongezeka,” alinukuliwa akisema na mashirika ya habari ya Urusi.

“Inasikitisha kwamba hawafanyi maamuzi ya busara.” Ryabkov alisema usalama wa nchi hizo mbili hautaimarika kutokana na hatua hiyo na kwamba Moscow itachukua hatua.

“Hawapaswi kujihadaa kwamba tutavumilia hili.” alisema.

Finland na Uswidi ziko tayari kujiunga na NATO kama ulinzi dhidi ya uvamizi unaohofiwa kutoka kwa Urusi.

Moscow imeionya Finland, nchi ambayo ina mpka na Urusi wa kilomita 1,300, kwamba itachukua ‘hatua za Madhubuti.”

Rais wa Ufini Sauli Niinisto alizungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumamosi kuhusu ombi la nchi hiyo kutaka uanachama wa NATO.

Ikulu ya Kremlin ilisema Putin aliona hatua ya Ufini kutoegemea upande wowote wa kijeshi kama ‘kosa.’

Finland ilitangaza nia yake ya kujiunga na NATO siku ya Jumapili huku chama tawala cha Uswidi kikisema kinaunga mkono uanachama, na hivyo kufungua njia ya kutuma maombi ya kujiunga na NATO.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted