DR Congo yaishutumu Rwanda kwa shambulio la waasi

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imelaumu kuzuka upya kwa ghasia za hivi karibuni za M23 kwa nchi jirani ya Rwanda, na kusababisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili...

0

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo liliishutumu Rwanda kwa kuunga mkono mashambulizi ya waasi wa M23 yaliyofanyiks siku ya Jumapili karibu na mji wa mpaka wa mashariki wa Bunagana, ambapo mapigano makali ya siku nzima yalisababisha mauaji ya wanajeshi wawili.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imelaumu kuzuka upya kwa ghasia za hivi karibuni za M23 kwa nchi jirani ya Rwanda, na kusababisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kudorora.

Rwanda imekanusha mara kwa mara kuunga mkono kundi la waasi.

Siku ya Jumapili, jeshi la Congo lilisema waasi wa M23 walishambulia maeneo karibu na Bunagana na maeneo mengine kadhaa ya jimbo la Kivu Kaskazini, “wakisaidiwa na wanajeshi na silaha kutoka kwa jeshi la Rwanda.”

Wanajeshi wawili waliuawa katika mapigano hayo, kwa mujibu wa taarifa, ambayo iliongeza kuwa wapiganaji kadhaa wa maadui pia waliuawa, bila kutaja takwimu.

Maafisa wa eneo hilo na maafisa wa jeshi waliambia AFP mapema Jumapili kwamba waasi wa M23 walikuwa wameanzisha mashambulizi ya asubuhi huko Bunagana ambapo jeshi lilikabiliana nalo.

Msemaji wa M23 Willy Ngoma pia alisema kuwa mapigano yalikuwa yakiendelea karibu na mji huo Jumapili jioni.

Waasi walikuwa wameshambulia maeneo karibu na mji huo, unaopakana na Uganda, mwezi Novemba 2021 na tena mwezi Machi.

Katika taarifa yake, jeshi la Congo lilisema Rwanda inalenga kuiteka Bunagana ili kuukabili mji mkuu wa jimbo la Goma na kuongeza shinikizo kwa serikali.

Uhusiano kati ya DRC na Rwanda umekuwa mbaya tangu kuwasili kwa Wahutu wa Rwanda mashariki mwa DRC wanaotuhumiwa kuwaua Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994.

Kundi la M23, ambalo kimsingi ni wanamgambo wa Kitutsi wa Congo, ni moja ya zaidi ya vikundi 120 vyenye silaha vilivyoko mashariki mwa DRC.

Iliiteka Goma kwa muda mfupi mwaka 2012 lakini mashambulizi ya pamoja ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na jeshi la Congo yalizima uasi huo.

M23 walianza tena mapigano mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuishutumu serikali ya Congo kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya mwaka 2009 ambapo jeshi lilipaswa kuwajumuisha wapiganaji wake.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted