Ebola Uganda: Majaribio ya chanjo kuanza ‘hivi karibuni’

Chanjo kadhaa ziko katika hatua mbalimbali za utengenezaji dhidi ya virusi hivi, mbili kati ya hizo zinaweza kuanza majaribio ya kliniki nchini Uganda katika wiki zijazo

0

Visa sitini na tatu vilivyothibitishwa na vinavyowezekana vimeripotiwa katika mlipuko wa Ebola nchini Uganda, vikiwemo vifo 29, kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema chanjo zilizotumika kuzuia milipuko ya hivi karibuni katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hazina ufanisi dhidi ya aina ya virusi vya Ebola vinavyosambaa nchini Uganda. Aliongezea kwa kusema mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini  Uganda unawaathiri wahudumu wa afya.

“Kufikia sasa, visa 63 vilivyothibitishwa na vinavyowezekana vimeripotiwa, ikiwa ni pamoja na vifo 29,” Tedros aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva siku ya Jumatano.

“Wahudumu 10 wa afya wameambukizwa na wanne wamefariki. Watu wanne wamepona na wanapata huduma.” Alisema WHO inaiunga mkono serikali ya Uganda katika kukabiliana na mlipuko huo ambao umeripotiwa katika wilaya nne.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limetoa dola milioni 2 kutoka mfuko wake wa dharura kwa ajili ya dharura na linashirikiana na washirika kusaidia wizara ya afya kwa kutuma wataalamu wa ziada, vifaa na rasilimali, Tedros alisema.

“Kunapokuwa na ucheleweshaji wa kugundua mlipuko wa Ebola, ni kawaida kwa visa kuongezeka kwa kasi mwanzoni na kisha kupungua kwani hatua za kuokoa maisha na hatua za kudhibiti mlipuko zinatekelezwa,” alisema.

“Chanjo zilizotumika kwa mafanikio kukabiliana na milipuko ya hivi karibuni ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hazina ufanisi dhidi ya aina ya virusi vya Ebola ambavyo vinahusika na mlipuko huu nchini Uganda.

“Hata hivyo, chanjo kadhaa ziko katika hatua mbalimbali za utengenezaji dhidi ya virusi hivi, mbili kati ya hizo zinaweza kuanza majaribio ya kliniki nchini Uganda katika wiki zijazo, zikisubiri idhini ya udhibiti na maadili kutoka kwa serikali ya Uganda.”

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted