Moshi ya bangi hudhuru mapafu zaidi kwa watumiaji wa sigara, utafiti wabaini

Bangi hatari na bandia kama K2 na Spice, haitumiwi sana katika majimbo ambayo bangi imehalalishwa.

0
(FILES) Mwanamke akivuta bangi wakati wa hafla ya kuhalalisha bangi eneo la Trinity Bellwoods Canada.

Kuvuta bangi wakati ukiwa mvutaji wa tumbaku kunaweza kuongeza zaidi uharibifu kwenye mfumo wa upumuaji, utafiti wa hivi punde umebaini.

Bangi hatari na bandia kama K2 na Spice, haitumiwi sana katika majimbo ambayo bangi imehalalishwa.

“Kuna dhana ya umma kwamba bangi ni salama kuliko tumbaku, na utafiti huu unazua wasiwasi kwamba huenda si kweli,” amesema mwandishi mkuu wa utafiti Dkt Giselle Revah, profesa msaidizi katika idara ya radiolojia katika chuo kikuu cha Ottawa huko Ontario nchini Canada.

“Muungano wa madaktari wa mapafu Marekani umesema kitu pekee ambacho kinapaswa kuingia kwenye mapafu yako ni hewa safi, kwa hivyo ikiwa unavuta kitu chochote, kinaweza kuwa sumu kwenye mapafu yako, “ amesema Revah.

Utafiti wa awali, uliochapishwa siku ya jumanne katika jarida la Marekani  kwa jina “Radiology”, ulilinganisha vipimo vya kifua vya kompyuta (CT) kutoka kwa watu 56 waliovuta bangi na tumbaku na uchunguzi wa mapafu wa watu 33 ambao walikuwa wavutaji sigara kwa zaidi ya miaka 25.

Vipimo kutoka kwa watu wengine 57 wasiovuta sigara bila ugonjwa wa mapafu, matibabu ya ugonjwa wa mapafu ama historia nyingine ya uharibifu wa mapafu vilitumika kama vidhibiti.

Kati ya watu asimilia 75 katika utafiti waliovuta bangi na sigara walikuwa na ugonjwa wa mapafu unaosababisha uharibifu wa mifuko ya hewa kwenye mapafu  huku asilimia 67 ya wanaotumia sigara pekee wakiwa na ugonjwa huo wa mapafu na asilimia 5 ya wasiotumia sigara wakiwa na ugonjwa wa mapafu.

Utafiti wa awali uliashiria uharibifu wa mapafu ulikuwa mkubwa zaidi kwa wale wanaovuta bangi na tumbaku ikilinganishwa na wavutaji tumbaku.

Kulingana na Revah, tofauti ya asilimia 8 kati ya bangi na tumbaku na wavutaji tumbaku inaweza kutoonekana kama tofauti kubwa lakini ilikuwa muhimu.

“Inapendekeza kwamba bangi ina athari za ziada kwenye mapafu kuliko tumbaku pekee.  Je! ni mchanganyiko wa bangi na sigara ambao husababisha mashimo zaidi kwenye mapafu na uvimbe kwenye njia ya hewa au bangi yenyewe tu?” alisema Revah.

Dkt Revah anasisitiza kuwa wasiwasi mwingine ulikuwa umri wa wavuta bangi kwani wengi walikuwa chini ya miaka 50.

Utafiti huo ulikuwa na mapungufu, Revah alibainisha. Ilikuwa ndogo. Kulikuwa na maelezo machache kuhusu kiasi cha bangi iliovutwa au jinsi ilivyovutwa.

Hata hivyo, kuna tofauti kadhaa kuhusu jinsi bangi na tumbaku zinatumiwa ambazo zinaweza kutoa dalili kwa uchunguzi zaidi. Kwa mfano, tumbaku kwa kawaida huvutwa na chujio, wakati bangi haivutwi na chujio.

Aidha, wavutaji tumbaku hupumua haraka, wakati wavutaji bangi mara nyingi huvuta na kushikilia pumzi yao ili kuongeza kiwango cha juu.

Utafiti wa mwaka 2021 uligundua kuwa vijana wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kuripoti kupumua au kupiga miluzi kifuani baada ya kuvuta bangi kuliko baada ya kuvuta sigara za aina yeyote.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted