Fahamu zaidi kuhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya Francis Ogolla aliyefariki katika ajali ya helikopta

Jenerali Ogolla, 61, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Ruto mnamo Aprili mwaka jana baada ya muda wa karibu miaka miwili kama naibu.

0

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Jenerali Francis Omondi Ogolla, na maafisa wengine tisa wa kijeshi walifariki katika ajali ya helikopta katika kaunti ya Elgeyo Marakwet, siku ya Alhamisi Aprili 18, 2024, Rais William Ruto alithibitisha kupitia mkutano na waandishi wa habari.

Rais Ruto ambaye alikuwa ameitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Kitaifa baada ya habari za ajali hiyo kuibuka, alisema wanajeshi wengine tisa waliokuwa ndani ya helikopta hiyo pia waliuawa huku wawili wakinusurika. Ruto alisema Jeshi la Anga la Kenya lilituma timu ya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Helikopta ya Ogolla ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka kijiji cha Chesegon, ambapo yeye na wasaidizi wake walikuwa wakitembelea shule baada ya kusimama katika maeneo mengine kuona wanajeshi wa Kenya na maeneo mengine.

Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Ijumaa, huku bendera rasmi zikipepea nusu mlingoti.

Miili ya wahasiriwa, ikiwa imepambwa kwa bendera za Kenya, ilirejeshwa Nairobi kwa ndege ya jeshi la anga siku ya Alhamisi.

Jenerali Ogolla, 61, alikuwa amekaa katika wadhifa huo mwaka mmoja pekee. Ogolla aliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Ruto mnamo Aprili mwaka jana baada ya muda wa karibu miaka miwili kama naibu.
Chini ya kanuni za kijeshi za Kenya, mkuu wa ulinzi kwa kawaida hustaafu akiwa na umri wa miaka 62 au baada ya miaka minne katika wadhifa huo, chochote kitakachotangulia.

Ruto aliwaambia wanahabari Mei mwaka jana kwamba alimteua Ogolla licha ya yeye kuwa miongoni mwa waliojaribu kubatilisha ushindi wake katika uchaguzi dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mwaka wa 2022.

“Nilipotazama wasifu wake, alikuwa mtu bora zaidi kuwa (a) jenerali,” Ruto alisema, akiongeza uamuzi wake ulikwenda kinyume na matakwa ya watu wengi.
Ogolla alijiunga na KDF mnamo Aprili 1984, akipanda ngazi hadi kama kamanda wa Jeshi la Wanahewa la Kenya mnamo 2018, wadhifa alioshikilia kwa miaka mitatu.


In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted