Asia Gamba
-

Tanzania kufanya marekebisho ya kodi kila baada ya miaka mitatu
Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa itakuwa inafanya marekebisho ya kodi kila baada ya miaka mitatu ili kuwa na Sera ya kodi inayotabirika na kuwafanya wawekezaji kuweka mipango yenye ufanisi.
-

Dola milioni 29.3 kutumika kuboresha mchakato wa ukusanyaji data za elimu Tanzania
Mkataba huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Marcias.
-

Mahakama ya Afrika Mashariki yatupilia mbali pingamizi la mradi wa bomba la mafuta
Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la kutaka kusimamisha ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye thamani ya $4bn (£3.1bn) kutoka Uganda hadi nchini Tanzania.
-

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, atuhumiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake
Gekul ambaye ni Mbunge wa Chama cha Mapinduzi CCM, anatuhumiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana wake kumwingizia chupa sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wake, Hashim Ally au kumpiga risasi kwa madai kwamba alitumwa kimkakati…
-

Tanzania yapiga hatua kupunguza vifo vya mama na mtoto
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya akinamama wajawazito kutoka vifo 556 556 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 mwaka 2022.
-

Waziri:Wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wasakwe
Pia Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni ameliagiza jeshi hilo litumie taarifa ilizonazo kuwatafuta na kuwakamata wanaojihusisha kutengeneza magobore na lifanye mapitio ya sheria na kanuni ili kuona kama iko haja ya kuzifanyia marekebisho.
-

Rufaa ya Sabaya na wenzake yakwama kusikilizwa
Leo Novemba 15, 2023 mahakamani hapo mjibu rufaa mmoja ambaye ni Sabaya pekee ndiye aliyekuwepo mahakamani, huku wajibu rufaa wenzake wawili wakidaiwa kuwa nje ya Arusha na wako njiani kurudi hivyo mahakama kuamua kuahirisha hadi…
-

Tanzania yatajwa kuwa kwenye kiwango kizuri cha upatikanaji wa Chakula
Tanzania imetajwa kuwa kwenye kiwango kizuri cha upatikanaji wa chakula kutokana na kuwepo kwa takwimu sahihi za hali ya Maisha katika kaya, hali iliyopelekea kiwango cha umasikini wa chakula kushuka nchini.
-

Whozu, Billnass na Mbosso wapunguziwa adhabu na BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapunguzia adhabu wasanii wa bongofleva nchini Tanzania, Whozu, Billnass na Mbosso na kuwataka wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa.
-

Watu wawili wafa maji mkoani Pwani
Matukio ya vifo hivyo yametokea kwa nyakati tofauti ikiwa ni sehemu ya madhara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.







