Bulaya:Mimi bado ni mwanachama wa Chadema
Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya amesisitiza kuwa yeye bado ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), isipokua suala la yeye kufukuzwa uanachama ni mambo ya ndani ya chama na ndio maana mpaka leo wanapigania haki yao ya kuwa wanachama wa Chadema.