TLS yasisitiza Utu, Upendo na Utii kuondoa migogoro ya kijamii
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi leo Jumanne Februari 18, 2025, kwenye Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Jijini Mwanza, ameshauri kuzingatiwa kwa Ibara ya Tisa ya Katiba ya Tanzania yenye kuhimiza kuhusu utu, Upendo na utii kama suluhu ya migogoro mingi ya kijamii.