Rais Samia awasili Ethiopia tayari kushiriki mkutano wa AU
Ziara ya Rais Samia nchini Ethiopia imeanza leo ambapo anatarajia kuhitimisha Februari 16,2025.
Ziara ya Rais Samia nchini Ethiopia imeanza leo ambapo anatarajia kuhitimisha Februari 16,2025.
Kiongozi wa upinzani wa Uganda, Kizza Besigye, anasema kuwa “anaumwa vibaya” gerezani siku tatu baada ya kuanza mgomo wa kula kupinga kizuizi chake, alieleza mmoja wa mawakili wake.
Imeelezwa kuwa jumla ya madereva bodaboda 759 wamefariki dunia kutokana na ajali za barabarani kati ya mwaka 2022 na 2024.
Malawi imetangaza kuwa inajiandaa kutoa vikosi vyake kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda limelizindua shambulizi jipya.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini Tanzania, Sheikh Issa Ponda, pamoja na viongozi wengine 11 wa Kiislam, ndio waliofungua kesi hiyo ya kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakipinga mamlaka ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) juu ya maamuzi yanayohusu masuala ya dini.
Hii leo inatajwa kwa ajili ya kuangaliwa iwapo upelelezi wa kesi umekamilika, ingawa imefungwa mikono kuendelea na hatua zaidi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kuwasilisha kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu kupatikana kwa dhamana ya mshtakiwa kutokana na kuangalia uhalali wa kesi ya jinai kwa haraka.
Milango ya kliniki ya LGBTQ ya OUT huko Johannesburg imefungwa kwa zaidi ya wiki moja na huduma za kinga na matibabu ya HIV zimefungwa kwa wateja wake 6,000.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwambukusi, amesema kuwa TLS siyo kikundi cha kigaidi bali ni taasisi halali inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa na haki ya kuishauri, kupongeza, na hata kuikosoa serikali pale inapobidi.
Mkutano huo ulifanyika baada ya wanajeshi 16 kutoka Afrika Kusini na Malawi, pia wanachama wa SADC, kuuawa katika mapigano ya karibuni karibu na Goma, ambako walikuwa wamepelekwa kama sehemu ya juhudi za kudumisha amani.
Salwan Momika aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake huko Södertälje, karibu na Stockholm, wakati akifanya matangazo ya moja kwa moja.