, , , , , ,

Mahakama Kuu yaamuru Kanja na Amin kufika mahakamani Jumanne kueleza aliko Mwaipaya

Victor Wanaswa Avatar

Mahakama Kuu nchini Kenya imewaamuru Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Upelelezi wa Makosi ya Jinai (DCI) Mohammed Amin kufika mahakamani wao wenyewe Siku ya Jumanne kuelezea aliko mwanaharakati wa Tanzania Twaha Mwaipaya ambaye aliripotiwa kutekwa nyara katika eneo la Kamulu Oktoba 25, 2026.

Jaji Alexander Muteti alitoa agizo hilo katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi, kufuatia wakaili Martha Karua kuitaka mahakama kuwalazimisha maafisa hao wakuu wa usalama kutoa maelezo kuhusu kutoweka kwa mwanaharakati huyo. Karua aliishutumu idara ya polisi kwa kutokuwa na haraka katika juhudi za kumtafuta Mwaipaya.

Akiwakilisha shirika la Vocal Afrika, Karua alisema kuwa jukumu la kueleza kutoweka kwa Mwaipaya haliwezi kukabidhiwa kwa maafisa wav yeo vya chini, akisisitiza kuwa maafisa wakuu zaidi wa usalama nchini wanapswa kufika mahakamani na kujibu maswali moja kwa moja.

Karua alitaka kujua kwa nini uchunguzi kuhusu kutoweka kwa mwanaharakati huyo unaonekana kuanza siku moja baadaye, licha ya polisi kuripotiwa kufahamishwa kuhusu tukio hilo mnamo Jumapili, Oktoba 25.

“Ni jukumu la polisi kuhakikisha usalama na ustawi wa Wakenya na watu wote walio ndani ya mipaka ya Kenya. Baada ya kufahamishwa kuhusu tukio hilo siku ya Jumapili, hawawezi kudai kuwa walianza uchunguzi siku ya Ijumaa, ispokuwa wanaiambia mahakama kuwa wameitelekeza kazi tunayowalipa kufanya,” alisema Karua mbele ya mahakama.

Karua pia aliwashutumu maafisa wa polisi kwa kukaidi agizo la awali la mahakama lililowataka kumfikisha Mwaipaya au mwili wake mbele ya mahakama.

“Tayari wamekaidi agizo la pili la mahakama. Hatuna Mwaipaya hapa wala mwili wake. Waje mbele yako na kuwajibikia kwa Wakenya, Watanzania na Waganda,” Karua aliiambia mahakama.

Wakili huyo mwandamizi pia alihoji kwa nini wachunguzi wanasubiri majibu kutoka kwa kampuni za mawasiliano za Safaricom na Aiitel ili kupata taarifa zinazoweza kusaidia kubaini aliko mwanaharakati huyo.

Alisema kuwa maafisa wa polisi wamewahi kudhihirisha uwezo wa kupata taarifa za mawasiliano ya simu wakati wa uchunguzi wa makosa ya jinai, akitoa mfano wa uchunguzi kuhusu mauaji ya Mbunge wa Kasipul Charle Ong’ondo Were.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Marwa alipinga ombi hilo akisema kuwa uchunguzi bado unaendelea na kwamba Mwaipaya hayuko mikononi mwa polisi.

Marwa aliiambia mahakama kuwa Kamishna wa polisi Kittony Pamoja na maafisa wakuu wa masuala ya sheria walikuwa wakiwakilisha Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi wa DCI.

Alisema kuwa wachunguzi walikuwa wameziandikia kampuni za Safaricom, Airtel na Bolt kuomba taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufuatilia aliko mwanaharakati huyo.

Serikali pia ilifichua kuwa mashahidi kadhaa, akiwemo mwenyeji wa Mwaipaya, James Gatunyi, walikuwa tayari wamerekodi taarifa zao kwa polisi. Hata hivyo, wachunguzi walikuwa bado hawajapokea majibu kutoka kwa kampuni hizo za mawasiliano.

 

 

 

 

 

 

Our Correspondent Avatar