Mashirka 16 ya Umma yaunganishwa,manne yafutwa
Serikali ya Tanzania imetangaza kuyaunganisha mashirika na taasisi 16 na kufuta mashirika na taasisi za umma nne, ili kuongeza tija katika utendaji kazi.
Serikali ya Tanzania imetangaza kuyaunganisha mashirika na taasisi 16 na kufuta mashirika na taasisi za umma nne, ili kuongeza tija katika utendaji kazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba alitangaza Alhamisi Desemba 14, 2023 kuwa Serikali ya Israel iliwafahamisha kuwa Joshua Mollel, kijana wa Kitanzania aliyekuwa akisoma nchini Israel, aliuawa mara baada ya kuchukuliwa mateka na kundi la Hamas. tarehe 07 Oktoba 2023.
Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam jana Desemba 14,2023, ilibatilisha uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kuwavua uanachama wabunge wa Viti Maalum, Halima Mdee na wenzake 18 ambao walituhumiwa kwenda Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama hicho
Mganga mkuu wa Serikali nchini Tanzania, Prof. Tumaini Nagu amewata wananchi kuzingatia kanuni za afya kwa kuzingatia usafi na kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa ukamilifu ili kujikinga na magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo mafua, kikohozi, kupumua kwa shida, kuwashwa koo, homa na kuumwa kichwa.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtu mmoja (32), akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka saba ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Nalunga, iliyopo katika Halmashauri ya Mji Nanyamba, mkoani hapa.
Mwanasheria wa haki za binadamu kutoka nchini Tanzania Joseph Moses Oleshangay ametunukiwa Tuzo ya Haki za Kibinadamu ya Weimar nchini Ujerumani mnamo Desemba 10, 2023, ambayo pia ilifanyika kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Kibinadamu, kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa.
Oleshangay, who comes from the Maasai community, has been campaigning against the government authorized expulsion of the Maasai for many years
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema Serikali itachukua hatua kwa waliomzushia kifo Makamu wa Rais, Dk Phillip Mpango, ili kudhibiti matumizi mabaya ya mtandao na kuwalinda wananchi dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao.
EWURA imesema kwa mwezi huu wa Desemba, 2023 bei za mafuta (FOB) kwenye soko la dunia zimepungua kwa wastani wa 0.8 kwa mafuta ya petroli na asilimia 9.11 kwa mafuta ya dizeli
Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa itakuwa inafanya marekebisho ya kodi kila baada ya miaka mitatu ili kuwa na Sera ya kodi inayotabirika na kuwafanya wawekezaji kuweka mipango yenye ufanisi.