Kesi ya Tundu Lissu yafutwa

Kesi ya Tundu Lissu yafutwa

0

Kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu pamoja na mwandishi wa habari mwandamizi Jabir Idrisa na wenzao wawili imefutwa na mahakama ya Hakimu mkazi Kisitu jijini Dar es salaam, baada ya upande wa serikali kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti hilo la Mawio Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jaman Ismail Mehboob.Lissu na wenzake walishtakiwa kwa makosa matano ikiwa ni pamoja na kuandika na kuchapisha habari ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari ‘’Machafuko yaja Zanzibar’’ kwenye gazeti la Mawio kinyume cha sheria ya magaezeti ya mwaka 2002.

Kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka 2016 jijini Dar es salaam washtakiwa Jabir Mkina na Lissu waliandika taarifa hiyo ya uchochezi.Katika shitaka la pili walidaiwa januari 14 mwaka 2016 walichapisha habari hizo za kuleta chuki visiwani Zanziabar.


Katika shitaka jingine mshtakiwa Mehboob alidaiwa kuchapisha gazeti hilo Januari 13 mwaka 2016 katika jengo la Jamana jijini Dar es salaam bila kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa msajili wa magazeti.Kesi hiyo imedumu kwa zaidi ya miaka mitano imefutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) Sylvester Mwakitalu chini ya sheria kifungu cha 91 cha sheria ya makosa ya jinai ambapo ameieleza mahakama upande wa jamhuri hauna nia ya kuendela na shauri hilo.Uamuzi wa kuifuta kesi hiyo, umetolewa leo, Septemba 22, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Joseph Luambano baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Wakili wa Serikali, Ashura Mzava ameieleza  mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Baada ya Mzava kueleza hayo, Hakimu Luambano amesema kupitia kifungu hicho, Mahakama imewafutia mashtaka washtakiwa wanne na kuwaachia huru.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted