Majeshi yaliyopindua serikali ya Guinea yametangaza mikakati itakayorudisha taifa katika uongozi wa raia.

mikakati hoyo itatumiwa kuunda katiba mpya na kufanyika kwa uchaguzi wa huru ,wazi na wa haki, ingawaje haikueleza serikali ya mpito itakuwepo kwa muda gani.

0
Luteni Kanali Mamady Doumbouya

Majeshi yaliyopindua serikali ya Guinea yametangaza mikakati itakayorudisha taifa katika uongozi wa raia.

Hati hiyo iliyosomwa kwenye runinga Jumatatu, imeeleza mikakati itakayotumiwa kuunda katiba mpya na kufanyika kwa uchaguzi wa huru , wazi na wa haki, ingawaje haikueleza serikali ya mpito itakuwepo kwa muda gani.

Majeshi yaliyoongozwa na Luteni Kanali Mamady Doumbouya, mnamo Septemba 5 yalimkamata Rais Alpha Conde (83) ambaye amekuwa akiiongoza taifa hilo la magaharibi mwa Afrika kwa miaka mingi.

Alpha Conde, ni rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Guinea mwaka 2010 na kuchaguliwa tena mwaka 2015. Ila mwaka jana alifanya mabadiliko ya katiba ambayo yalimpa nafasi ya kuwania urais kwa muhula wa tatu mwezi Oktoba 2020.

Hatua hiyo ilizua maandamano na machafuko ambapo watu kadhaa walipoteza maisha yao. Conde alishinda uchaguzi wa mwaka 2020 ila vyama vya upinzani vilipinga vikali ushindi huo.

Alpha Conde, Rais wa Guinea

Hati mpya inabainisha taasisi nne ambazo zitasimamia mabadiliko hayo.

Kamati ya kitaifa ya maendeleo (CNRD) itakayobuniwa na junta na kuongozwa na Doumbaya; itajumuisha taasisi nne ikiwemo; rais wa mpito atakayekuwa kiongozi wa kamati ya National Rallying Committee for Development (CNRD); mkuu wa nchi na mkuu wa majeshi; serikali itakayoongozwa na Waziri mkuu; na bodi ya kutunga sheria iitwayo National Transition Council (CNT) Baraza la kitaifa la mpito.

Wanachama wa taasisi hizi hawataruhusiwa kushiriki uchaguzi wowote nchini humo katika kipindi hiki cha mpito.

Kipindi cha mpito, “kitaamuliwa baada ya makubaliano kati ya viongozi tofauti nchini” kulingana na hati hiyo mpya.

Mataifa jirani na Guinea, wanachama wa jumuiya ya mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS wanawasiwasi na msukosuko wa kisiasa nchini humo,Guinea ikiwa moja wapo ya mataifa maskini zaidi Afrika.

Mapinduzi ya Guinea yakiwa ya pili katika kipindi cha miezi 13 baada ya mapinduzi ya Mali.

ECOWAS inataka uchaguzi ufanyike ndani ya miezi sita, na kuachiwa kwa Conde.

Balozi wa Guinea katika Umoja wa Mataifa, aliiambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatatu kuwa hati za uchaguzi zitabadilishwa na katiba mpya itatungwa kabla kufanyika kwa uchaguzi.

Baraza la kitaifa la Mpito (CNT) linalojumuisha wanachama 81 kutoka vyama tofauti vya kisiasa, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, waajiri, vikosi vya usalama na vyombo vingine wanajukumu la kuunda katiba mpya.

Wanachama wa serikali ya conde na wale kutoka taasisi za uongozi wa Conde hawatajumuishwa kwenye baraza hilo la mpito.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted