Desmond Tutu, Prince Philip na DMX kati ya watu mashuhuri walioaga dunia mwaka wa 2021

Kuanzia kwa Mwanamfalme Philip wa Uingereza hadi mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Desmond Tutu, hawa ni baadhi ya watu mashuhuri walioaga dunia mwaka wa 2021.

0
Mwanamfalme Philip wa Uingereza

Kuanzia kwa Mwanamfalme Philip wa Uingereza hadi mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Desmond Tutu, hawa ni baadhi ya watu mashuhuri walioaga dunia mwaka wa 2021.

Januari

Mtangazaji mashuhuri nchini Amerika Larry King, aliyewahi kuwahoji watu wengi tu mashuhuri kutoka mataifa tofauti aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87.

– Febuari

Rais wa zamani wa Argentina Carlos Menem alifariki akiwa na umri wa miaka 90 Februari 14.

“Baba wa taifa” la Papua New Guinea Sir Michael Somare, waziri mkuu wake wa kwanza, alifariki akiwa na umri wa miaka 84 mnamo Februari 26.

– Machi

Nguli wa muziki wa Reggae Bunny Wailer alifariki Machi 2 akiwa na umri wa miaka 73.

Mfalme wa Wazulu wa Afrika Kusini Goodwill Zwelithini, 72, alifariki Machi 12.

Kiongozi wa zamani wa Madagascar Didier Ratsiraka, mchochezi wa mapinduzi ya kisoshalisti katika kisiwa cha Bahari ya Hindi, alifariki akiwa na umri wa miaka 84 Machi 28.

– Aprili –

Mwanamfalme Philip, Duke wa Edinburgh, aliyekuwa mumewe Malkia Elizabeth II wa Uingereza, alifariki Aprili 9 akiwa na umri wa miaka 99.

Rapa wa Marekani DMX alifariki siku hiyo hiyo akiwa na umri wa miaka 50.

DMX,Rapa wa Amerika

Bernie Madoff, mpangaji mkuu wa kashfa kubwa zaidi ya kifedha katika historia, alifariki dunia akiwa jela huko North Carolina Aprili 14 akiwa na umri wa miaka 82.

Rais wa Chad Idriss Deby, 68, alifariki kutokana na majeraha aliyopate vitani siku moja baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa sita Aprili 20.

– Mei

Kiongozi wa Boko Haram nchini Nigeria, Abubakar Shekau, ambaye umri wake haukujulikani, aliuawa wakati wa mapigano kati ya makundi hasimu ya kundi hilo la itikadi kali Mei 19.

– Juni-

Rais mwanzilishi wa Zambia Kenneth Kaunda aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 97 mwezi Juni 17.

– Julai

Richard Donner, mwelekezi  wa filamu ya kwanza ya “Superman” alifariki Julai 5 akiwa na umri wa miaka 91.

Siku mbili baadaye nyota wa Bollywood aliyependwa sana Dilip Kumar aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 98.

– Agosti

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre alfariki kutokana na Covid-19 akiwa na umri wa miaka 79. Alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela nchini Senegal kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Jacques Rogge, rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, alifariki Agosti 29. Mbelgiji huyo alikuwa na umri wa miaka 79.

– Septemba

 Rais wa muda mrefu zaidi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika alifariki Septemba 17 akiwa na umri wa miaka 84.

 Oktoba 

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia nchini Kenya Agnes Tirop, 25, aliuawa kwa kuchomwa kisu nyumbani kwake Oktoba 13. Mumewe baadaye alishtakiwa kwa mauaji yake.

Colin Powell, shujaa wa vita na waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa Marekani Mweusi ambaye sifa yake ilichafuliwa kutokana na uvamizi wa Iraq, alifariki Oktoba 18 akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua UVIKO-19.

– Novemba

FW de Klerk, rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini, alifariki akiwa na umri wa miaka 85 mnamo Novemba 11. Alimwachilia Nelson Mandela kutoka gerezani na baadaye kushinda naye Tuzo ya Amani ya Nobel.

Mwandishi wa riwaya mzaliwa wa Zambia Wilbur Smith, 88, ambaye aliandika matukio ya ajabu katika bara la Afrika, aliaaga dunia siku mbili baadaye.

– Decemba –

Lamine Diack, ambaye aliongoza riadha ya kimataifa kutoka 1999 hadi 2015 lakini baadaye akapatikana na hatia ya rushwa, alifariki Desemba 3 akiwa na umri wa miaka 88.

Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu, mwanaharakati aliyepinga ubaguzi wa rangi na ukosefu wa haki kote duniani aliaga dunia Desemba 26 akiwa na umri wa miaka 90.

Desmond Tutu, Kasisi na mwanaharakati
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted