Ghasia katika mji wa magharibi mwa Cameroon watatiza michuano ya AFCON

Makundi yenye silaha yalikuwa yameonya kabla ya kuanza kwa AFCON kwamba yanapanga kuvuruga michuano hiyo.

0

Wanajeshi na watu wenye silaha wameshambuliana kwa risasi katika jiji la Cameroon la Buea, na kuwaacha watu kadhaa na majeraha katika mji mkuu wa eneo lililokumbwa na ghasia za watu waliojitenga.

Makabiliano hayo yalifanyika katika mji ambao ni wa wachezaji wa timu tofauti zinazishiriki katika katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), meya wa eneo hilo alisema Alhamisi.

“Vikosi vya usalama viliingilia kati kwa haraka na uchunguzi unaendelea kubaini ni nani aliyehusika,” Meya David Mafani Namange aliambia AFP.

Mapema Alhamisi, afisa mkuu wa kijeshi alisema kwa njia ya simu kwamba mapigano “yalitokea baada ya kikosi cha Mali kumaliza mazoezi,” na kuongeza: “Hayakuwa athiri mazoezi ya timu za AFCON”.

Afisa mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) alipuuza tukio hilo, na hakuna vyombo vya habari vya kitaifa vya Cameroon vilivyoripoti kulihusu.

“Tunajua kwamba kulikuwa na mtafaruku, lakini hatujui hata kidogo ni nini hasa kilichotokea, ikiwa kulikuwa na shambulio au la,” afisa huyo wa CAF aliambia AFP, akiomba kutotajwa jina.

Mamlaka, iliyofikiwa na AFP, ilikataa kuthibitisha rasmi au kukana kwamba kulikuwa na tukio lolote.

Siku ya Jumatano, seneta wa upinzani alipatikana ameuawa baada ya kupigwa risasi katika eneo hilo, kulingana na chama chake

Mbunge Henry Kemende wa Social Democratic Front (SDF), mojawapo ya vyama vikuu vya upinzani nchini Cameroon, alikuwa amepigwa risasi kadhaa kifuani, kulingana na makamu wa rais wa SDF, Joshua Osih.

Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji hayo, lakini Osih aliwalaumu makundi ya watu wanaotaka kujitenga.

Rais Paul Biya ameshutumiwa kwa kukandamiza upinzani katika maeneo yanayozungumza Kiingereza pamoja na kuwabana sana wapinzani wa kisiasa.

Akielezea kuhusu ghasia za Jumatano, mwanasheria wa haki za binadamu, Agbor Balla, aliiambia AFP “Kulikuwa na majibizano makali ya risasi kati ya wanajeshi na wanaotaka kujitenga.”

Makundi yenye silaha yalikuwa yameonya kabla ya kuanza kwa AFCON Jumapili iliyopita kwamba yanapanga kuvuruga michuano hiyo.

Timu zilizo katika Kundi F — Tunisia, Mali, Mauritania na Gambia — zinafanya mazoezi mjini Buea na kucheza katika eneo la pwani la Limbe.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted