Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio ya hivi punde

Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 1.7 wameikimbia Ukraine, na kuufanya mzozo huu kuwa mkubwa zaidi na unaokuwa kwa kasi zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia.

0

Haya hapa ni matukio ya hivi punde katika vita vya Urusi nchini Ukraine:

Mpango mpya wa kuwahamisha watu

Urusi inasema itafungua njia maalum za wakimbizi wanaotoroka mashambulizi nchini Ukraine. Njia hizo zitafunguliwa kuanzia mwendo wa saa 0700 GMT siku ya Jumanne ili kuruhusu raia kuhama kutoka miji kadhaa ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Kyiv na mji wa bandari wa Mariupol.

Ukraine inaorodhesha njia za uokoaji kutoka Kyiv pamoja na Mariupol, Kharkiv na Sumy — zote zimekuwa chini ya mashambulizi makubwa ya Urusi katika siku za hivi karibuni.

Hakuna wanajeshi wa kujiandikisha: Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin anasema hawapeleki askari au askari wa akiba kupigana na kwamba askari wataalamu watatimiza malengo maalum katika vita nchini Ukraine.

Urusi inavuruga uhamishaji

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anaishutumu Urusi kwa kupuuza uhamishwaji wa raia kupitia njia za kibinadamu kwa kutumia vifaru, virusha roketi na vilipuzi.

Urusi haijasonga zaidi katika mashambulizi yake

Urusi imetumia karibu nguvu zake zote za kivita na kuziweka katuka mpaka wa Ukraine, Pentagon inasema.

Vikosi vya Urusi “kwa kweli havijafanya maendeleo yoyote kwenye mashambuli yake dhidi ya Ukraine katika siku chache zilizopita,” msemaji wa Pentagon John Kirby anasema.

Matokeo ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi

Mshauri wa rais wa Ukraine anasema duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi kwenye mpaka wa Belarus na Poland ilileta “matokeo chanya” katika kufungua njia salama kwa wakimbizi.

Hata hivyo, mpatanishi mkuu wa Urusi Vladimir Medinsky anasema matarajio ya Moscow kutokana na mazungumzo hayo ‘hayakutimia’.

Uturuki imetangaza kuwa itawakaribisha mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Ukraine kwa mazungumzo Alhamisi.

Baadhi ya viongozi kutoka Ukraine na wa Urusi katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo. Mazungumzo yalifanyika mnamo Machi 7, 2022. (Photo by Maxim GUCHEK / BELTA / AFP) /

Wakimbizi wapigwa makombora wakikimbia –

Urusi inaongeza mashambulizi ya makombora katika miji, pamoja na mji wa Gostomel karibu na Kyiv, Kharkiv mashariki, Sumy kaskazini mashariki, Chernihiv kaskazini na Mykolayiv kusini magharibi.

Makumi kwa maelfu bado wamenaswa kwenye vita hivyo wakiwa bila maji wala umeme katika bandari ya kusini ya Mariupol baada ya majaribio mawili ya kuwahamisha kutofaulu.

Waapa kuiadhibu zaidi Urusi

Viongozi wa Amerika, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza waapa “kuendelea kuongeza gharama kwa Urusi” kutokana na uvamizi wake dhidi ya Ukraini, Ikulu ya White House inasema baada ya mazungumzo kwenye mtandao wa simu.

Duka la kuoka mikate lashambuliwa

Takriban watu 13 wameuawa kwa kushambuliwa kwa makombora katika duka la viwandani huko Makariv, karibu kilomita 50 magharibi mwa Kyiv, huduma za uokoaji za Ukraine zilisema.

Mapigano makali karibu na Kyiv

Wanajeshi wa Kiukreni na wakaazi wanaokimbia wanaelezea kuhusu mapigano makali kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi mwa Kyiv, ikijumuisha mapigano ya mitaani na mapigano ya mtu kwa mwinhine ambayo yanaweza kuenea hivi karibuni hadi mji mkuu uliozingirwa.

Mwanamke ashikilia bango wakati wa maandamano ya “Women stand with Ukraine” mjini Brussels, mnamo Machi 8, 2022. (Photo by ERIC LALMAND / various sources / AFP) / Belgium OUT

Wanasoka wa kigeni waruhusiwa kuondoka Urusi

Wanasoka na makocha wa kigeni wanaofanya kazi Urusi na Ukraine wataruhusiwa kusimamisha kandarasi zao kwa muda na kuhamia kwingine, FIFA yatangaza.

Mashirika ya michezo yameizuia Urusi kushiriki mashindano ya kimataifa kufuatia uvamizi wa Ukraine na FIFA inasema hatua hizo mpya ziliundwa “kuwezesha kuondoka kwa wachezaji wa kigeni na makocha kutoka Urusi” ikiwa wanataka kuondoka.

Umoja wa Mataifa unatafuta njia ya kutoa wa misaada salama

Umoja wa Mataifa unahitaji njia salama ili kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo yenye migogoro nchini Ukraine, afisa mkuu ameliambia Baraza la Usalama.

Raia katika maeneo kama Mariupol, Kharkiv, Melitopol na kwingineko wanahitaji sana misaada, hasa vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha, “Naibu katibu mkuu wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths ameuambia mkutano wa dharura.

Bei ya mafuta na gesi yapanda

Bei ya mafuta ilipanda zaidi kupita miaka 14 iliyopita, na bei ya gesi asilia Ulaya na Uingereza ikafikia viwango vya juu baada ya Amerika kupendekeza kuwekewa vikwazo kwa uagizaji wa mafuta kutoka nchini Urusi.

Viongozi wa Ujerumani, Uingereza na Uholanzi wanaonya dhidi ya marufuku hiyo, hata hivyo, wakisema inaweza kuweka usalama wa nishati barani Ulaya hatarini.

Bei ya nikeli, ambayo Urusi ni mzalishaji mkuu, inapanda kwa asilimia 90 kufikia rekodi ya juu, juu ya hofu ya usambazaji.

Madeni yanayolipwa kwa kutumia rubles

Urusi inasema itaruhusu makampuni ya Kirusi na watu binafsi kulipa madeni kwa wadai wao katika mataifa ‘hasama’ ikiwa ni pamoja na Amerika, EU, Uingereza, Kanada na Japan, kwa fedha za Urusi Ruble.

Warusi wahitaji nguo: Uniqlo

Kampuni kubwa ya nguo ya Japan Uniqlo yatetea uamuzi wake wa kuacha maduka yake wazi nchini Urusi, ikizingatiwa kuwa wapinzani wao Zara na H&M walisimamisha shughuli zao nchini humo kutokana na kushambuliwa kwa Ukraine.

“Mavazi ni hitaji la kimsingi,” anasema Tadashi Yanai, rais wa kampuni ya Uniqlo Fast Retailing.

Wakimbizi milioni 1.7

Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 1.7 wameikimbia Ukraine, na kuufanya mzozo huu kuwa mkubwa zaidi na unaokuwa kwa kasi zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Wakimbizi wa Ukraine wakisubiri kuabiri gari kuenda Ujerumani ,mnamo Machi 08, 2022. (Photo by Louisa GOULIAMAKI / AFP)
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted