Misri yawasilisha malalamiko kuhusu tabia ya mashabiki baada ya kupoteza mechi yao na Senegal

Siku ya Jumanne, Pharoahs wa Misri walikosa nafasi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar baada ya kushindwa na Senegal katika Uwanja wa michezo wa Diamniadio huko Dakar.

0

Shirikisho la Soka la Misri (EFA) limewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya shikisho la Senegal kwa vurugu na “ubaguzi wa rangi” kutoka kwa mashabiki, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano.

Siku ya Jumanne, Pharoahs wa Misri walikosa nafasi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar baada ya kushindwa na Senegal katika Uwanja wa michezo wa Diamniadio huko Dakar.

Kwa mujibu wa taarifa ya EFA, “timu ya Misri ilikabiliwa na ubaguzi wa rangi huku umati wa watu wakinyanyua mabango ya kuudhi kwenye viwanja, hasa dhidi ya nahodha wa timu Mohamed Salah.”

Malalamiko hayo pia yalihusisha wachezaji kurushiwa chupa za maji na mawe wakati wa mazoezi.

Picha zilizotolewa na EFA zinaonyesha vioo vya basi lililowabeba wachezaji wa Misri vikiwa vimevunjwa, mabango ya matusi dhidi ya Salah, na mashabiki wa Senegal wakitoa ishara chafu kwa wachezaji.

Pamoja na malalamiko hayo rasmi, mitandao ya kijamii nchini Misri imefurika picha za uso wa mshambuliaji wa Liverpool, Salah ukiwa umefichwa na viashiria vingi vya laser ya kijani alipokuwa akipiga penalti.

Mashabiki wengi wa Misri wamelaumu Salah kukosa kufungwa bao kutokana na leza zilizomulikwa usoni mwake, ingawa wengine wameeleza kuwa mashabiki wa Misri mara nyingi hutumia mbinu hiyo dhidi ya timu zinazozuru mjini Cairo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted